Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide
Mwongozo wa Mkufunzi
Mungu Roho Mtakatifu Kuna kweli chache za kitheolojia katika historia ya Kanisa ambazo zimezua mabishano mengi, kutokubaliana, na mafarakano kama fundisho la Roho Mtakatifu. Kuanzia mabishano ya zamani kuhusu Utatu na fundisho la “procession” (yaani fundisho kuhusu nafsi ipi ya Utatu iliipeleka nafsi nyingine kutenda kazi) hadi kutokubaliana kwa siku za leo kuhusiana na ubatizo na karama za Roho Mtakatifu, kuna mengi ambayo yanaweza kutufanya tuliendee somo hili kwa tahadhari; lakini, ninatumai kwa dhati kwamba haitakuwa hivyo. Fundisho la Roho Mtakatifu ni kiini cha uelewa wetu kuhusu asili ya Mungu na namna tunavyoweza kuuishi uwepo wake hai katikati yetu. Moduli hii inaangazia Nafsi na Kazi ya Roho Mtakatifu, ikianza na ushahidi wa kibiblia wa Mungu Roho Mtakatifu kama nafsi ya tatu ya Mungu mmoja aliye katika Utatu. Tunaanza somo letu kwa kuchunguza kile ambacho Biblia inaonyesha kuhusu Roho kama nafsi ya kiungu ambaye ni Mungu na anatenda kwa ufahamu kama Mungu. Pia tutazungumzia uhusiano wa Roho na Baba na Mwana, ambapo Yeye ni “Kifungo cha Upendo” kati yao na “Zawadi yao ya Upendo kwa Ulimwengu.” Kisha, tutaangazia asili ya ufunuo wa kinabii na kweli kwamba Roho ndiye anayevuvia na kuangazia Neno la Mungu, na kuwahakikisha wanadamu kwa habari ya dhambi, akituwezesha kushinda udanganyifu unaosababishwa na dhambi na kutuongoza kwenye toba ya kweli. Tunafunga somo letu kwa kuangalia kwa kina uwepo wenye nguvu wa Roho Mtakatifu, yaani, huduma yake ya neema na nguvu katika maisha ya wale wanaotubu na kuamini. Tutaelezea jukumu muhimu la Roho katika tendo kuzaliwa upya, kuasiliwa (kufanywa wana), ubatizo, karama, kukaa ndani mwamini, kutia muhuri, na utakaso. Hakika, Roho Mtakatifu analiwezesha Kanisa kutimiza utume wake ulimwenguni.
Terry Cornett (B.S., M. A., M.A.R.) ni Mwalimu wa Taaluma wa Heshima (Dean Emeritus) katika Taasisi ya The Urban Ministry huko Wichita, Kansas. Ana Shahada kadhaa kutoka katika Chuo Kikuu cha Texas huko Austin, Chuo cha Wheaton Graduate School, na Chuo cha Theolojia cha C. P. Haggard katika Chuo Kikuu cha Azusa Pacific. TUMI imejitolea kuwezesha vuguvugu za upandaji makanisa kote ulimwenguni ambazo zinawaandaa viongozi ili kuendeleza Ufalme miongoni mwa watu maskini wa mijini. World Impact ni shirika la kimisheni la Kikristo ambalo limejidhatiti kuwezesha harakati za upandaji makanisa kwa njia ya kufanya uinjilisti, kuandaa na kuwawezesha maskini wa mijini wa Amerika. Maono yetu ni kuandikisha, kuwawezesha, na kuwatuma viongozi wa mijini ambao watapanda makanisa na kuzindua harakati za upandaji makanisa ya kienyeji.
kuandaa viongozi. kuwezesha harakati.
THE URBAN MINISTRY INSTITUTE • HUDUMA YA WORLD IMPACT, INC.
Made with FlippingBook - Share PDF online