Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide

1 1 0 /

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

³ Kazi ya Roho Mtakatifu ya kuzaa upya hutufanya kuwa hai lakini sio kukomaa. Kama vile kuzaliwa kwa mwanadamu kunafuatiwa na hitaji la kukua kuelekea ukomavu, vivyo hivyo kuzaliwa kiroho pia kunafuatiwa na hitaji la kukua katika Kristo. ³ Kazi ya Roho Mtakatifu ya kututengeneza upya mtu mmoja mmoja ni sehemu ya kazi yake kubwa ya kufanya mambo yote kuwa mapya. Roho Mtakatifu anafanya kazi ili kutimiza mpango mkuu wa Mungu wa kuumba mbingu mpya na nchi mpya ambamo vitu vyote vitawekwa huru kutokana na madhara ya dhambi. ³ Kwa sababu ya dhambi ya baba yetu Adamu, kwa asili sisi ni “wana wa ghadhabu” na hatuwezi kudai kuwa watoto wa Mungu kwa namna yoyote ya asili. Roho Mtakatifu huwaasili waamini katika familia ya Mungu wakati wanapoweka imani yao kwa Kristo na, kwa neema kabisa, huwapa haki na urithi wa watoto wa kifalme. Tendo hili la kufanywa kuwa wana hutuhakikishia urafiki wa kipekee na Mungu na pia kuadibishwa na kurekebishwa tunapokosa kumtii. ³ Huduma ya Roho Mtakatifu ya kufanya wana inatukumbusha kwamba wokovu hauwezi kamwe kutenganishwa na mahusiano na Kanisa. Kumpokea Kristo siku zote kunahusisha kuasiliwa katika familia yake (Kanisa) na hivyo hakuna anayeokolewa ili awe nje ya familia nzima ya Mungu. ³ Mojawapo ya kazi muhimu zaidi za Roho Mtakatifu katika wokovu ni kazi yake ya kutuunganisha na Kristo ili kwamba nguvu za maisha ya Yesu, kifo, ufufuo, na kupaa kwake zihesabiwe kwetu na kuanza kufanya kazi ndani yetu. Mapokeo ya makanisa ya Reformed yanasisitiza kwamba hili hutokea wakati Roho Mtakatifu anayeishi ndani yetu anapofanya uwepo wa Kristo kuwa halisi katika maisha yetu na yanaiita kazi hii ya ubatizo katika Roho Mtakatifu kufuatia maneno ya Paulo kuhusu Roho ambaye anatubatiza katika Mwili wa Kristo. ³ Wakristo wengi wa Kiprotestanti ambao hawako katika mapokeo ya makanisa ya Reformed wanapendelea kutumia neno “ubatizo katika Roho Mtakatifu” wakirejelea tukio linalofuata baada ya kuupokea wokovu. Badala ya kuunganisha ubatizo wa Roho na uwepo wa Roho (kama mapokeo ya makanisa ya Reformed yanavyoamini), Waprotestanti hawa wanamfuata mwandishi Luka katika kusisitiza ubatizo wa Roho kama tukio maalum la kupokea nguvu za Mungu.

3

Made with FlippingBook - Share PDF online