Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide

1 2 0 /

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

I. Roho Anayetoa Karama

Muhtasari wa Sehemu ya 1 ya Video

A. Kwanini karama za rohoni ni za lazima? Nguvu kwa ajili ya kushuhudia.

ukurasa 261  2

1. Matendo 1:8 – Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu RohoMtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.

2. Kusudi la Kanisa ni kuwa mashahidi kwa kile ambacho Mungu amefanya, na anafanya, katika ulimwengu, na nguvu kwa ajili ya kulikamilisha jukumu hili inatoka kwa Roho Mtakatifu. Roho anatupa karama ili kwamba tuwe jamii inayoeneza Habari Njema kwa ufanisi ya kwamba Yesu ndiye Bwana wa vitu vyote. Hata kwa zile karama ambazo zinafanya kazi ndani ya Kanisa tu na ni kwa wale ambao tayari wanamjua Kristo, bado zinakusudi hilohilo. Roho anatoa karama ili kuliimarisha Kanisa na washirika wake, lakini sababu kubwa ya Kanisa kuimarishwa ni ili liwe na nguvu ya kukamilisha kusudi lake ulimwenguni.

4

B. Karama za rohoni ni nini?

ukurasa 263  3

1. Neno Charisma: Neema ya Mungu inayofanya kazi ndani yetu na kupitia sisi.

a. Neno ambalo linatumika zaidi likitafsiriwa kama “karama za rohoni” ni neno la Kiyunani charisma. Neno hili linatokana na neno la Kiyunani lenye maana ya neema yaani ( charis ) na maana yake halisi ni “karama za neema.” Kulingana na Warumi 5:15 16, wokovu wenyewe unaonekana kuwa ndiyo karama ya kuu (ya msingi) ya neema—karama ambayo katika hiyo karama nyingine zote huchipua. Lakini neno charisma au karama za rohoni linatumika kimahususi zaidi katika vifungu kadhaa vya Maandiko katika Agano Jipya.

Made with FlippingBook - Share PDF online