Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide

1 2 8 /

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

(3) 1 Wakorintho 12:11 (4) 1 Wakorintho 7:7

b. Karama hazihusiani na hadhi ya mtu, 1 Kor. 12:20-22.

3. Kuwa na karama fulani ya rohoni hakuamui kiwango cha kiroho cha mtu.

ukurasa 267  7

a. 1 Wakorintho 13: kipimo halisi cha kiwango cha kiroho cha mtu si karama, bali ni upendo. 1 Wakorintho 13 inaonyesha kwamba dhumuni la msingi la Roho kukaa ndani yetu ni utimilifu katika Upendo. Kwa mujibu wa ufahamu wa Paulo, utendaji kazi wa karama ambao haulengi kutimiza kusudi hili si utendaji “wa Roho.” Hakuna tendo la nguvu (kama ishara, miujiza) linaloweza (lenyewe tu) kuthibisha kazi ya Roho kama ambavyo tendo moja la upendo linaweza kufanya. b. Hadithi ya Baalamu (Hesabu 22-24) Mwonaji Baalamu alitembea katika uwepo ulio hai wa Roho wa Mungu uliokuwa ukimjia kwa namna ya ajabu kiasi kwamba alikuwa anatabiri chini ya upako wa kiungu (Hes. 24:2-3), na akaweza hata kuona kwa usahihi kabisa ujio wa Masihi wa Mungu ambaye angekuja wakati wa baadaye sana (Hes. 24:17). Lakini Mtume Petro anasema kwamba katika vipimo vya Mungu Baalamu alikuwa mtu “aliependa njia za udhalimu” (2 Pet. 2:15). Karama za rohoni zinatumika kwa usahihi na mtu aliyekomaa kiroho katika kukamilisha makusudi ya Mungu lakini, karama zenyewe hazina chochote kinachoweza kumfanya mtu akomae kiroho. c. Sisi sote tu “vyombo vya udongo,” 2 Kor. 4:7. Udhihirisho wa nguvu za Mungu na uwepo wake si suala la kiroho chetu bali ni neema yake. Hakuna hata mmoja anayestahili karama za neema ya Mungu.

4

Made with FlippingBook - Share PDF online