Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide
/ 1 3 5
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
3. Hatua tatu za utakaso Mchakato wa utakaso unahusisha hatua tatu: kutenga, kutakasa, na kukamilisha. Utakaso unahusiana na mwanzo [kutengwa], muendelezo [kutakaswa], na lengo [kukamilishwa] kwa maisha ya Kikristo. Hivyo utakaso ni tendo la wakati uliopita, uliopo, na ujao. ~ J. Rodman Williams. Renewal Theology. a. Wanatheolojia mara nyingi hutumia maneno matatu tofauti kufafanua mchakato huu unaoendelea wa kutengwa kwa ajili ya Mungu. Maneno hayo ni kuhesabiwa haki, kutakaswa, na kutukuzwa. Kwa hiyo tunaweza kusema mambo matatu kwa wakati mmoja: sisi tuliotakaswa [tukiwa tumetengwa kwa ajili ya Mungu], tunatakaswa [tunatengwa kwa ajili ya Mungu], na tutatakaswa [tutatengwa kwa ajili ya Mungu]. (1) Mwanzo [kutengwa] - KUHESABIWA HAKI (a) Matendo 26:18; Warumi 5:9; Wagalatia 2:16 (b) ZINGATIA: Kuhesabiwa haki kunamaanisha kwamba tunatangazwa na Mungu mwenyewe kuwa wenye haki. Hii inamaanisha kwamba Mungu hatuhesabii tena dhambi zetu dhidi yetu bali anahesabu kwamba kifo cha Kristo kwa ajili ya dhambi kililipia adhabu yetu kikamilifu. Kifo hicho kinafuta uasi wetu uliopita na kututenga na ulimwengu kama watu ambao hawapaswi tena kukabiliana na ghadhabu ya Mungu dhidi ya dhambi. Kuhesabiwa haki ni hatua ya kwanza ya lazima katika mchakato wa utakaso [kutengwa kwa ajili ya Mungu]. Soma 1 Kor. 1:2; Ebr. 10:14. (2) Muendelezo [kutakaswa] - UTAKASO (a) Warumi 6:19; 1 Thes. 5:23 (b) Z INGATIA: Kuwa na Roho hutufundisha sisi kuishi kama ambavyo Kristo aliishi, ili kwamba matendo na tabia zetu ziendelee kuakisi utakatifu zaidi na zaidi; hicho ndicho ambacho mara nyingi tunaita mchakato wa utakaso katika maisha ya kila siku. Kama ambavyo mwanatheolojia mmoja anavyoliweka hilo kwa usahihi kwa kusema, matumizi ya kawaida zaidi ya neno utakaso
ukurasa 268 9
4
Made with FlippingBook - Share PDF online