Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide
1 4 8 /
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
Nimetiwa Sahihi, Nimetiwa Muhuri, Nimekombolewa, Mimi ni Wako !
Kila mchungaji wakati fulani huulizwa swali hili: “Nitajuaje kwamba nina uzima wa milele?” Mtu anayeuliza swali hili anaweza kuwa muumini mpya kabisa, lakini pia anaweza kuwa mtu ambaye amekuwa mshirika wa kanisa kwa miaka mingi. Kwa kawaida ni kwa sababu anapambana na mashambulizi ya Shetani ambayo yanaweza kujumuisha mashaka, hatia na shutuma za ndani, na hata vita dhidi ya dhambi zinazomsumbua. Ungejibuje swali hilo? Roho Mtakatifu daima yuko kazini kuwaandaa watu wa Mungu kwa ajili ya kazi za huduma na ushuhudiaji. Katika somo hili tumezungumza namna ambavyo Roho anavyowastahilisha kwa ajili ya huduma/ushuhudiaji kwa kuwatenga na kuwafananisha na sura ya Kristo (utakaso). Tumeangalia namna ambavyo Roho anawawezesha kwa ajili ya huduma/ushuhudiaji kwa kudhihirisha nguvu zake kupitia wao (kuwapa karama za rohoni). Na hatimaye, tumeona namna ambavyo Roho anawawezesha watu wa Mungu kustahimili na kudumu katika huduma/ ushuhudiaji kwa kuwatia muhuri na kuwapa uhakikisho wa uwepo wa Mungu unaowawezesha kusonga mbele wakikabiliana na mashaka na kutokuwa na uhakika. Ikiwa unapenda kujifunza kwa kina zaidi baadhi ya mawazo kuhusiana na Uwepo Wenye Nguvu wa Roho Mtakatifu (Sehemu ya Pili), tafadhali soma vitabu hivi: Leslie B. Flynn. 19 Gifts of the Holy Spirit. Wheaton, IL: Victor Books, 1994. Harley H. Schmitt. Many Gifts, One Lord. Fairfax, VA: Xulon Press, 2002. Alexander, Donald L, ed. Christian Spirituality: Five Views of Sanctification. Downers Grove, IL: InterVarsity Press, 1989. Sasa utawajibika kutumia maarifa uliyoyapata katika moduli hii kwa vitendo kwa njia ambayo wewe na mkufunzi wako mtakubaliana. Fundisho hili kuhusiana na Roho Mtakatifu na kazi zake lina mambo mengi yaliyojaa utajiri mwingi ndani yake. Fikiria kuhusu namna zote ambazo fundisho hili linaweza kuathiri maisha yako ya ibada, maombi yako, mwitikio wako kwa kanisa lako, mtazamo wako kazini, na mengine mengi. Jambo muhimu ni kwamba uangalie namna ya kuhusianisha fundisho hili na maisha yako, kazi, na huduma. Kazi ya Huduma imeakusudiwa hasa kwa ajili ya hili, na katika siku za usoni utapata nafasi ya kuwashirikisha wengine maarifa haya katika maisha halisi, kwenye mazingira halisi ya huduma. Omba kwamba Mungu
3
Marejeo ya Tasnifu ya Somo
Nyezo na bibliografia
4
Kuhusianisha somo na huduma
Made with FlippingBook - Share PDF online