Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide

/ 1 8 1

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

Mifano ya Matamko ya Kimadhahebu kuhusu “Ubatizo katika Roho Mtakatifu” (muendelezo)

kumwamini Kristo Yesu. Kisha wanafunzi hawa wakabatizwa kwa maji, na kisha Paulo akaweka mikono juu yao na Roho Mtakatifu akaja juu yao. Muda ulikuwa mfupi kati ya wanafunzi hawa kumwamini Kristo na kuja kwa Roho Mtakatifu juu yao, lakini ulikuwa ni muda wa kutosha kwao kubatizwa katika maji. Ubatizo katika Roho ulikuwa tofauti na ulifuata baada ya wokovu. Ubatizo katika Roho sio kusudi kuu, lakini ni njia ya kufikia kusudi hilo. Kanuni ya kimaandiko kwa mwamini ni kujazwa na Roho daima. Ubatizo ni uzoefu wa kipekee ambao humtambulisha mwamini katika mchakato wa kuishi maisha yaliyojaa Roho. Ushahidi wa awali wa kimwili wa Ubatizo unahusu ishara ya kwanza ya nje kwamba Roho Mtakatifu amekuja kwa nguvu ijazayo. Uchunguzi wa Maandiko unaonyesha kulikuwa na ishara ya kimwili ambayo iliwapa watazamaji kutambua kwamba waamini walikuwa wamebatizwa katika Roho Mtakatifu. Ushahidi daima ulitokea wakati ule ule waamini walipobatizwa katika Roho na si katika tukio fulani la baadaye. Katika nyumba ya Kornelio kulikuwa na ushahidi wa kusadikisha kwamba Roho Mtakatifu alimwagwa juu ya watu wa mataifa (Matendo 10:44-48). Baadaye, Petro alipoitwa kuwaeleza viongozi wa kanisa la Yerusalemu kuhusu huduma yake katika nyumba ya Kornelio, alirejelea ushahidi unaoonekana wa waamini kubatizwa katika Roho Mtakatifu. Alitaja hilo kuwa sababu iliyomfanya awaandae waamini hao kwa ajili ya ubatizo wa maji (Matendo 11:15-17). Ingawa kunena kwa lugha kuna thamani ya kwanza ya uthibitisho, kumekusudiwa na Mungu kuwa zaidi ya uthibitisho wa uzoefu wa zamani. Pia kunaendelea kuleta utajiri kwa mwamini mmoja mmoja katika ibada binafsi, na kwa mkutano kunapoambatana na tafsiri ya lugha. Kanisa la Church of God in Christ Imetolewa kutoka katika Fundisho la Kanisa la Church of God in Christ, http://www.cogic.org/doctrnes.htm Tunaamini kwamba Ubatizo wa Roho Mtakatifu ni uzoefu unaofuata baada ya uongofu na utakaso na kwamba kunena kwa lugha ni matokeo ya ubatizo wa Roho Mtakatifu pamoja na madhihirisho ya tunda la Roho (Wagalatia 5:22-23; Matendo 10:46, 19:1-6). Tunaamini kwamba hatubatizwi kwa Roho Mtakatifu ili tupate kuokolewa (Matendo 19:1-6; Yohana 3:5). Mtu anapopokea ubatizo wa Roho Mtakatifu, tunaamini kuwa atazungumza kwa lugha isiyojulikana kwake kulingana

Mtazamo Mchanganyiko: Pentekoste-Holiness

Made with FlippingBook - Share PDF online