Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide
1 8 8 /
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
K I A M B A T I S H O C H A 1 9 Maeneo Ambayo Wakristo Wanatofautiana Kuhusiana na Karama za Rohoni Mch. Terry G. Cornett
I. Kuna uhusiano gani kati ya “vipaji au uwezo wa asili” na “karama za rohoni”?
A. Mtazamo wa 1 – Karama za rohoni ni vile vipawa na uwezo wa asili uliojificha ndani ya kila mwanadamu, ambavyo huonekana pale unapotiwa nguvu, kuimarishwa, kupanuliwa, na kupewa mwelekeo mpya na Roho wa Mungu pale anapomzaa upya mtu. Mtazamo huu unakusudia kulinda ukweli kwamba:
1. Hakuna ukomo kati ya utendaji wa Roho anayeumba na anayeumba upya. (Wokovu ni urejeshaji wa asili na kutufanya kuwa wanadamu kamili kama tulivyokusudiwa kuwa tulipoumbwa).
2. Kwamba Mungu amechagua kufanyia kazi karama zake kupitia wanadamu ambazo ni pamoja na kutumia akili, miili na nafsi zao. Anatuhusisha katika kazi yake ili kwamba ingawa nguvu zake zitatuwezesha kufanya mengi zaidi ya mambo ya kibinadamu tu, bado zinafanya kazi ndani yetu, pamoja nasi, na kupitia sisi kama tulivyo.
3. Mungu alitujua sisi kabla na alikuwa akifanya kazi kabla ya wokovu wetu (taz. Yer. 1:5).
a. Yeremia 1:5 – Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.
Made with FlippingBook - Share PDF online