Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide

/ 3 5

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

B. Yamkini namna bora ya kumwelezea Roho Mtakatifu kama anavyoelezewa katika Maandiko ya Agano la Kale ingeweza kuwa “Pumzi ya Mungu yenye nguvu.”

1. Katika Maandiko ya Kiebrania, Pumzi ya Mungu ni nguvu yenye uwezo ambayo inaharibu (Kut. 15:10; Isa. 11:4) na kuumba (Zab. 33:6).

ukurasa 239  22

1

Neno la Kiebrania linalotafsiriwa kama ‘roho ’ ni ruach . Mzizi wa neno r-w ch , ambako nomino hiyo imechipukia, maana ya kwanza kabisa ni “kupumua kwa nguvu kutumia pua.”... Neno ruach linatafsiriwa kama kupumua kwa nguvu kubwa, kwa vurugu, ambapo hapa ni kinyume cha neno neshamah , ambalo kwa kawaida linamaanisha, kupumua kwa utulivu.... Neno ruach linatumika mara kwa mara kama upepo; kama mara themanini na saba kwa jumla. Katika hizi, thelethini na saba zinaongelea upepo kama wakala wa Yehova, ambapo mara nyingi ni upepo ule unaoharibu, na mara zote ni upepo mkali na wenye nguvu.... ruach-adonai [Roho wa Bwana] ni udhihirisho wa uweza wa Mungu uletao uzima na nguvu katika maisha ya mwanadamu..... ruach-adonai hawezi kuzuiwa (hafungwi), bali ni kama neno lake, ambalo halitamrudia Yeye bure, bali litatimiza apendalo. ~ N. H. Snaith. Chapter VII, “The Spirit of God.” The Distinctive Ideas of the Old Testament . kurasa za 143-158.

2. Dini ya Kiyahudi katika Agano la Kale ilimuelewa Roho Mtakatifu kuwa ni “nguvu ya Mungu inayotenda kazi.” Nguvu hiyo inadhihirika kama:

ukurasa 240  23

a. Nguvu katika vita (kama vile upepo wa Mungu unavyoonekana ukiigawanya bahari ya Shamu au pale ambapo Waamuzi wanatiwa nguvu katika mapigano yao dhidi ya maadui wa Israeli).

b. Aina mbalimbali za hekima (kama wale mafundi katika kuijenga Hema ya Bwana au Yusufu au Danieli wakiwa na vipawa maalum kwa ajili ya usimamizi wa Serikali).

Made with FlippingBook - Share PDF online