Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide
3 8 /
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
(2) Yohana 7:37-39 (3) Yohana 4:14 (4) 1 Wakorintho 6:11 (linganisha na Tito 3:5) (5) Ufunuo 22:17
Tazama Ray Pritchard, Names of the Holy Spirit . Chicago: Moody Press, 1995. kurasa za 57, 69, 77, 100, 187.
b. Mafuta – utegemezaji wa maisha. Katika nyakati za kibiblia, mafuta ya zeituni yalitumiwa kwa ajili ya chakula na dawa na vile vile kama nishati za taa ambazo ziliwashwa ili kutoa mwanga ndani ya nyumba. Mafuta hayo yalikuwa muhimu sana katika maisha ya kila siku kiasi kwamba yalikuwa ni ishara ya ustawi. Mtu asingeweza kufikiria mafuta bila kufikiria uponyaji, usalama na utele. Yalitegemeza maisha. Mafuta kama mfano wa Roho Mtakatifu, yalichukua jukumu muhimu zaidi kama ishara kwa sababu ya matumizi ya kibiblia ya upako [yaani kutia mafuta]. Manabii (1 Wafalme 19:16), Makuhani (Kut. 28:41), na Wafalme (2 Sam. 2:4; 1 Wafalme 1:34) walikuwa wakipakwa mafuta ili kuwatenga kwa ajili ya huduma. Kumiminwa huku kwa mafuta kulikuwa ni ishara ambayo ilionyesha waziwazi kwamba mtu huyo alikuwa ana Roho Mtakatifu juu yake. Kutiwa mafuta kulionyesha kwamba Mungu alikuwa amemchagua na kumtayarisha mtu ili kuwahudumia watu wake afya, usalama, na utele. Katika Maandiko ya Agano la Kale upako huu maalum wa mafuta (kutiwa nguvu) wa Roho Mtakatifu kwa kawaida ulifanyika kwa wale tu waliohudumu kama manabii, makuhani, au wafalme. Katika Agano Jipya, kila mwamini katika Kristo, anapokea upako wa Roho Mtakatifu kuwa mhudumu wa uzima kwa wengine. (1) 1 Samweli 16:13a (linganisha na Isa. 61:1). (2) Luka 4:18 (3) 2 Wakorintho 1:21-22 (4) 1 Yohana 2:20 & 27 (linganisha na Yohana 14:26)
1
Ibid. uk. 19.
Made with FlippingBook - Share PDF online