Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide
/ 4 5
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
japokuwa si muhimu sana, lakini bado inamjumuisha yeye mzima” ( Lessons In Truth, H. Emilie Cady , kilichochapishwa na The Unity School of Christianity, kurasa za 18, 19-20). Mara moja unatambua kwamba amekuwa akijifunza na kikundi ambacho hakina fundisho sahihi la Mungu au Utatu. Utamwambia nini Sue, na hicho kikundi cha mafunzo ya Biblia, unapozijibu nukuu alizozisoma?
Kutafuta Usahihi.
Carlos ni mwamini mpya katika Kristo ambaye anajaribu kuelewa kile ambacho Biblia inafundisha kuhusu Roho Mtakatifu. Anasema, “Ni rahisi kwangu kuelewa Yesu ni nani. Ninaweza kusoma hadithi kumhusu katika Maandiko na kujua yale hasa aliyosema na kufanya. Nilipoweka tumaini langu katika Kristo kwa ajili ya wokovu, nilihisi kama Petro alivyohisi alipomwambia Bwana kwamba hangeweza kwenda popote pengine kwa sababu Yesu alikuwa na “maneno ya uzima wa milele.” Lakini Roho Mtakatifu anaonekana kuwa fumbo kubwa sana. Siwezi kufikiria jinsi alivyo na sina uhakika ni jinsi gani ninapaswa kuwa na uhusiano naye. Unaweza kunisaidia kujua?” Je, unawezaje kutumia ufahamu wa sasa wa Carlos kuhusu Yesu ili kumsaidia kumwelewa Roho Mtakatifu? Makanisa mengi ya Kikristo yanafuata Kalenda ya Kanisa, yakitenga siku na majira maalum ili kusisitiza matukio muhimu yaliyomo katika Vitabu vya Injili na Kitabu cha Matendo ya Mitume. Fikiria kama kanisa lako lingekuwa linaadhimisha Jumapili ya Pentekoste* kwa mara ya kwanza kabisa. Katika mapokeo yenu, je, kuna nyimbo, matamko ya baraka, matendo, mapambo, rangi, alama, maandishi, utolewaji wa karama za rohoni, au aina nyingine za ibada ambazo zina msisitizo maalum juu ya Nafsi na kazi ya Roho Mtakatifu? Ikiwa ungewekwa kuwa msimamizi wa ibada hiyo ya Jumapili ya Pentekoste, ni mambo gani ungeweza kupanga ambayo yangelisaidia kusanyiko lako kumwabudu kwa furaha na kumtukuza Mungu Roho Mtakatifu? *Jumapili ya Pentekoste ni Jumapili ya 7 baada ya Pasaka, na kwa kawaida ni ibada inayoadhimisha na kusherehekea kuja kwa Roho Mtakatifu katika kutimiza unabii wa Yoeli (Yoeli 2:28-32) na ahadi ya Yesu (Yohana 14:16-17; 16:7; ; Matendo ya Mitume 1:8). Kuongoza Ibada ya Utatu.
2
1
ukurasa 242 29
3
Roho Mtakatifu ni Bwana; Nafsi ya tatu ya Mungu mmoja aliye katika Utatu. Yeye ni nafsi tofauti na Nafsi zingine za Uungu Matakatifu, anafikiri, kutenda, na kupenda kikamilifu kama Baba na Mwana na anashiriki kikamilifu Asili yao
Marejeo ya Tasnifu ya Somo
Made with FlippingBook - Share PDF online