Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide
/ 4 7
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
yake Yeye “anayeishi katika nuru isiyoweza kufikiwa.” Nifundishe maana ya Maandiko uliyoyavuvia. Niangazie akili yangu ili nipate kuijua kweli na kufahamu kile unachotaka nifanye kwa habari ya kweli hiyo. Nipe uwezo wa kutimiza wito wangu wa huduma. Nipe hekima ya kuwaongoza wengine katika maarifa yako ya kweli. Haya yote nayaomba kwa njia ya Yesu Kristo, anayeishi na kutawala pamoja nawe na Baba Mwenyezi, Mungu mmoja, aliyebarikiwa milele. Amina.
MAZOEZI
Warumi 8:15-17
Kukariri Maandiko
1
Ili kujiandaa kwa ajili ya kipindi, tafadhali tembelea www.tumi.org/books kupata kazi ya usomaji ya wiki ijayo, au muulize Mkufunzi wako.
Kazi ya usomaji
Wiki ijayo kutakuwa na jaribio (mtihani mdogo) kuhusiana na maudhui (yaliyomo kwenye video) ya somo hili wiki ijayo. Hakikisha kwamba unatumia muda wa kutosha kupitia maelezo uliyoandika katika daftari lako. Zingatia zaidi mawazo makuu ya somo. Soma maeneo uliyoagizwa, na uandike muhtasari usiozidi aya moja au mbili kwa kila eneo uliloagizwa kusoma. Katika muhtasari huo tafadhali eleza kile ambacho kwa uelewa wako kilikuwa wazo kuu la kila eneo au kitabu ulichosoma. Usijitaabishe kutoa maelezo mengi; andika tu kile unachoona kuwa wazo kuu linalozungumziwa katika sehemu hiyo ya kitabu. Tafadhali hakikisha unakuja na muhtasari huo darasani wiki ijayo. (Angalia “ Fomu ya Ripoti ya Usomaji ” mwishoni mwa somo hili). Katika somo letu linalofuata tutaangazia kazi ya kinabii ya Roho Mtakatifu. Tutazungumza kuhusu Neno la kinabii kama msingi wa kumjua Mungu na kuchunguza kazi ya Roho katika kuvuvia na kuangazia Maandiko. Tutaona kwamba Roho si tu kwamba nafanya kazi ya kinabii katika kulifunua Neno laMungu, bali kwa namna hiyo hiyo ndiye anayeliweka Neno la kinabii katika moyo wa mwanadamu. Tutaangalia huduma ya Roho Mtakatifu kuhusiana na kuwashuhudia watu kwa habari ya dhambi na kuwaleta kwenye toba. Katika haya yote tutathibitisha namna ambavyo tunamtegemea Yeye pekee kwa ajili ya kupatia ujuzi wa Mungu uletao wokovu na kupokea uwezesho wa kulitii kwa Neno lake.
Kazi nyingine
ukurasa 243 31
Kuelekea Somo Linalofuata.
Made with FlippingBook - Share PDF online