Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide

/ 5 1

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

Kazi ya Kinabii ya Roho Mtakatifu

S O M O L A 2

ukurasa 245  1

Karibu katika Jina imara la Yesu Kristo! Baada ya kusoma kwako, kujifunza, kufanya majadiliano, na kuweka katika vitendo maarifa yaliyomo katika somo hili, utakuwa na uwezo wa: • Kuelezea dhana ya kibiblia ya unabii. • Kuelewa kwamba Maandiko yote ni Neno la “kinabii” kutoka kwa Roho wa Mungu. • Kuona kwamba unabii wote unahusisha “kutangaza” ujumbe kutoka kwa Mungu kwa ajili ya mambo ya nyakati za sasa (forthtelling) , ilhali baadhi ya unabii pia unahusisha “kutabiri” tukio la wakati ujao katika mpango wa Mungu. • Kuonyesha kutoka katika Maandiko kwamba unabii ni huduma [karama] inayotolewa kwa wanawake na wanaume. • Kuthibitisha kutoka katika Maandiko kwamba unabii huja kupitia huduma ya Roho Mtakatifu. • Kuthibitisha madai ya kibiblia kwamba Roho Mtakatifu ndiye mwandishi wa Maandiko. • Kufafanua mafundisho ya uvuvio na kuangaziwa (kutiwa nuru ) na uhusiano kati ya dhana hizo. • Kutambua kwamba wanadamu wamedanganywa kuhusu hali yao ya dhambi (uzito na matokeo yake) na hivyo kutotaka na kutoweza kumtafuta Mungu na haki yake kwa ukweli wa mioyo yao. • Kueleza maana ya kuhakikisha na kufafanua kazi ya Roho katika kuwaleta watu kwenye ujuzi wa hali yao ya dhambi. • Kufafanua maneno ya Msingi ya Kiebrania na Kiyunani yanayo maanisha toba. • Kuelezea aina za mabadiliko yanayoambatana na toba ya kweli ya kibiblia. • Kuonyesha kutoka katika Maandiko kwamba toba ni matokeo ya kazi ya Roho Mtakatifu.

Malengo ya Somo

2

Made with FlippingBook - Share PDF online