Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide
/ 6 5
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
Kusudi letu la sehemu hii, Roho Anayetuhakikisha kwa Habari ya Dhambi Zetu , ni kukuwezesha wewe: • Kutambua kwamba wanadamu wamedanganywa kuhusu hali yao ya dhambi (uzito na matokeo yake) na hivyo kutotaka na kutoweza kumtafuta Mungu na haki yake kwa ukweli wa mioyo yao. • Kueleza maana ya kuhakikisha na kufafanua kazi ya Roho katika kuwaleta watu kwenye ujuzi wa hali yao ya dhambi. • Kufafanua maneno ya Msingi ya Kiebrania na Kiyunani yanayo maanisha toba. • Kuelezea aina za mabadiliko yanayoambatana na toba ya kweli ya kibiblia. • Kuonyesha kutoka katika Maandiko kwamba toba ni matokeo ya kazi ya Roho Mtakatifu.
Warumi 3:9-11 Ni nini basi? Tu bora kuliko wengine? La! Hata kidogo. Kwa maana tumekwisha kuwashitaki Wayahudi na Wayunani ya kwamba pia wamekuwa chini ya dhambi; 10 kama ilivyoandikwa, ya kwamba, Hakuna mwenye haki hata mmoja. 11 Hakuna afahamuye; Hakuna amtafutaye Mungu.
2
I. Huduma ya Roho Mtakatifu ya Kuhakikisha.
Muhtasari wa Sehemu ya 2 ya Video
A. Ufafanuzi: kuhakikisha ni kazi ya Roho ambayo inaleta uelewa wa ndani wa hatia mbele za Mungu. Inatengeneza uhakika wa ndani kwamba mtu ni mdhambi na kumfanya kutambua kwamba anastahili hukumu kutokana na matendo yake. Uhakikishaji huu unadhoofisha hali ya kujihesabia haki na kutoa visingizio vinavyoambatana na makosa ya kibinadamu. Hili linaelezewa vizuri sana kupitia maneno ya Isaya nabii aliyesema: “Ole wangu! Kwa maana nimepotea; kwa sababu mimi ni mtu mwenye midomo michafu, nami ninakaa kati ya watu wenye midomo michafu; na macho yangu yamemwona Mfalme, Bwana wa majeshi” (Isa. 6:5).
Roho Mtakatifu anaushinda upofu wa kiroho wa jamii ya wanadamu: kwanza, kwa njia ya kuwahakikisha kwa habari ya dhambi, jambo ambalo kwa njia ya Roho Mtakatifu humfufua mwenye dhambi ili apate ufahamu wa dhambi; na, pili, kwa njia ya neema ya toba, ambayo kwayo Roho humwongoza mtu kwenye huzuni ya kimungu kwa sababu ya dhambi. Huzuni hii ndiyo inayopelekea katika kuungama na kubadilika.
B. Uhakikishaji wa kweli wa dhambi kamwe si jambo la kibinadamu bali daima ni kazi ya Roho wa Mungu.
1. Moyo wa mwanadmu ni mdanganyifu, mwovu, na hauwezi kutambua hitaji lake kwa Mungu (Mwa. 3:13; 6:5; Zab. 14:1-3; Zab. 36:1-2; Isa. 29:13; Yer. 9:6-8; Rum. 3:10-18; 2 Kor. 4:3-4; 2 Tim. 3:12-13).
ukurasa 249 10
Made with FlippingBook - Share PDF online