Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide

/ 6 7

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

a. Neno la Kiebrania shubh- linamaanisha “kugeuka” au “kurejea.”

b. Ezekieli 14:6 – Kwasababu hiyo uwaambie nyumba ya Israeli, Bwana MUNGU asema hivi; Rudini ninyi[ shubh ], mkageuke na kuviacha vinyago nyenu; mkageuze nyuso zenu zisielekee machukizo yenu yote.

c. Neno hili linatuambia kwamba mtu anayetubu hupokea badiliko kubwa la mtazamo ambalo humfanya “kugeuka,” kufikiri na kutenda kwa njia tofauti kabisa.

2

2. Agano Jipya

a. Neno la kiyunani metanoia kimsingi linamaanisha “badiliko la nia.”

Neno Metanoia linaashiria badiliko kubwa la nia na moyo likifuatiwa na kujengwa kwa tabia mpya kutoka kwenye maisha ya dhambi, huzuni kwa ajili ya dhambi ili kuachana nayo kabisa. ~ Thomas C. Oden. Life in the Spirit . Systematic Theology: Volume Three. uk. 86.

b. 2 Petro 3:9 – Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyodhani anakawia, bali huwavumilia, maana hapendi mtu yeyote apotee, bali wote wafikie toba [ metanoia ].

c. Kama linavyotumiwa katika Maandiko, ni neno lenye uzito na utajiri mkubwa ambalo linaweza kutamkwa vyema kama badiliko la kusudi. Badiliko hili la kusudi linahusu maneno yote ya maisha ya mwanadamu .

B. Mabadiliko yanayojumuishwa katika toba ya kweli

1. Toba inayojumuisha badilko la NIA.

a. Kabla ya toba akili zetu zilimfikiria Mungu kama adui na kutuongoza kwenye matendo maovu (Kol. 1:21-22).

Made with FlippingBook - Share PDF online