Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide

8 4 /

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

Uwepo Wenye Nguvu wa Roho Mtakatifu (Sehemu ya Kwanza) Sehemu ya 1: Roho Anayezaa Upya na Kufanya Wana.

YALIYOMO

Mch. Terry G. Cornett

Lengo la sehemu hii ni kuonyesha jinsi Roho Mtakatifu huleta wokovu wa Mungu kwetu kwa kutufanya kuwa watu wapya kabisa na kutuweka katika familia ya Mungu. Baada ya kujifunza sehemu hii tunapaswa kuelewa kwamba: • Tunapookoka, Mungu hutubadilisha kwa njia ya Roho Mtakatifu. • Kwa sababu ya kazi ya “kuzaa upya” ya Roho Mtakatifu katika wokovu, tunabadilishwa na kuwa watu wapya, wenye uwezo mpya wa kumsikia na kumtii Mungu. • Kwa njia ya Roho Mtakatifu, Mungu hutukaribia wakati wa kuokoka kwetu, na kutuasili katika familia ya Mungu, na kutufanya tuelewe kwamba Mungu ni Baba yetu mwenye upendo. • Roho Mtakatifu hutubatiza katika Kristo Yesu, akituunganisha naye katika kifo na ufufuo wake.

Muhtasari wa Sehemu ya 1

3

I. Neno la Kiakrostiki RABBIS

Muhtasari wa Sehemu ya 1 ya Video

Neno la kiingereza RABBIS (wingi wa neno Rabbi wa Kiyahudi) litatumika katika kusaidia kukumbuka kazi ya Roho Mtakatifu katika maisha yetu.

A. Katikamapokeo yaKiyahudi, rabbi alikuwamtu aliyeidhinishwa kufundisha Maandiko na kueleza jinsi watu wanavyopaswa kuyatumia katika maisha yao. Vivyo hivyo Roho Mtakatifu ndiye mwalimu na mshauri wetu wa kiungu ambaye hutufunulia Kweli ya Mungu na pia hutuonyesha wazi jinsi tunavyoweza kuishi maisha yanayompendeza Mungu. B. Katika akrosti hii, kila herufi ya neno RABBIS inasimama kuelezea kazi maalumu ya Roho Mtakatifu katika maisha yetu. Kazi ya Roho Mtakatifu inajumuisha: (zimewekwa katika Lugha ya Kiswahili na Kiingereza ili kukusaidia kuona namna akrosti hii RABBIS ilivyotumika kuelezea kazi za Roho Mtakatifu katika maisha ya mwamini).

Made with FlippingBook - Share PDF online