Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide

9 4 /

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

Hitimisho

» Tunapookoka, Roho Mtakatifu anatuzaa upya (anatufanya watu wapya) ili tuwe na shauku na uwezo wa kumtii Mungu. » Tunapookoka, Roho Mtakatifu hutufanya wana na kutuingiza katika familia ya Mungu ili tuweze kukaa daima katika uwepo wake, tuhudumiwe kama watoto wa kiume na wa kike wa Mungu, na kujiungamanisha na familia ya Mungu ambayo ni kanisa.

Maswali yaliyo hapa chini yameandaliwa ili kukusaidia kutambua mambo muhimu katika sehemu yetu ya mwisho ya video kuhusu “Roho Anayezaa Upya na Kufanya Wana.” Tafadhali jibu maswali yafuatayo kwa umakini, uwazi na kwa ufupi, na inapowezekana, jenga hoja kwa kutumia Maandiko! 1. Neno “kuzaliwa upya” linamaanisha nini? 2. Kuna tofauti gani kati ya kuhesabiwa haki na kuzaliwa upya? 3. Je, ni baadhi ya maneno gani mengine yaliyotumika katika Maandiko kufafanua dhana ya kuzaliwa upya? 4. Kuna uhusiano gani kati ya kazi ya Mwana wa Mungu na kazi ya Roho Mtakatifu wa Mungu katika tendo la kuzaliwa upya kwa mtu? 5. Zaidi ya kufanywa upya kwa mtu mmoja-mmoja, ni nini kingine ambacho Biblia inafundisha kwamba Mungu atakifanya upya? 6. Kwa nini fundisho la kufanywa wana ni la lazima? 7. Ni uthibitisho gani unaoonyesha kwamba mtu amepokea “Roho ya kufanywa wana”? 8. Ni haki na wajibu gani huja baada ya kufanywa wana katika familia ya Mungu? 9. Kwa kuzingatia uhusiano wenye nguvu kati ya “maisha mapya” na “kuzaliwa upya” katika tendo la kuzaliwa upya, makanisa yanahitaji kufanya mambo gani ili kuwalea na kuwalinda wale ambao ni wakristo wapya?

Sehemu ya 1

Maswali kwa wanafunzi na majibu

3

Made with FlippingBook - Share PDF online