Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide
/ 9 9
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
(2) Kupitia ubatizo wa Roho tunaingizwa katika Kanisa. (a) 1 Wakorintho 12:13 (b) Waefeso 2:19-22 (c) 1 Wakorintho 3:16-17 – Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu? 17 Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi.
III. Ubatizo katika Roho Mtakatifu: Kuelewa Maeneo ambayo Wakristo Hawakubaliani
A. Njia mbili tofauti za kuelewa namna Roho Mtakatifu anavyokuja kwetu
3
1. Ubatizo wa Roho kama Tendo la Mara Moja Tu. Mtazamo huu unaamini kwamba Roho Mtakatifu na kazi yake yote ndani ya mwamini hupokelewa pale tu mtu anapookoka na kwamba maisha yote ya ukristo ni utendaji (au kukua katika) kile kilichopokelewa wakati huo. Kwa mtazamo huu, kazi ya Roho Mtakatifu katika maisha ya mtu baada ya wokovu kimsingi inaendelea hatua kwa hatua. 2. Ubatizo wa Roho kama tendo lenye hatua nyingi. Mtazamo huu unaamini kwamba Roho Mtakatifu anapokelewa katika hatua mbili au zaidi na ambazo zinajumuisha tukio tofauti na mahususi baada ya wokovu ambalo huleta “ubatizo wa Roho.” Kwa maneno mengine, wakati Roho Mtakatifu anapokelewa wakati wa wokovu, kuna kazi maalum za Roho Mtakatifu ambazo hupokelewa baadaye. Katika theolojia hizi, neno “ubatizo katika Roho Mtakatifu” mara nyingi humaanisha utendaji (kazi maalum za uwezeshaji kwa ajili ya huduma au ushindi juu ya dhambi) ambao huja baadaye badala ya kuelezea ujio wa kwanza wa Roho pale mtu anapookoka.
Made with FlippingBook - Share PDF online