The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide
/ 1 0 1
UFALME WA MUNGU
1. Kutufariji kuhusu kufiwa na wapendwa wetu
a. Mahusia ya Paulo kwa Wathesalonike, 1 The. 4
b. Waamini, kwa sababu ya utimilifu wa Ufalme, hawahitaji kuhuzunika kama waliopotea, ambao hawana tumaini la utawala wa Mungu kurudi katika nguvu duniani.
Ingawa waamini wanaweza kufa
kimwili katika enzi hii, tumaini letu ni la hakika kabisa kwamba kwa wakati na namna yake, Bwana atatimiza ahadi yake kupitia manabii na mitume ya kutawala milele kama Mfalme, katika mbingu mpya na nchi mpya ambapo haki na kweli yake vitadumu milele.
c. Paulo anawaelekeza Wathesalonike katika kweli za kurudi kwa Yesu, kisha anahasa kwamba wafarijiane kwa maneno hayo, 1 Thes. 4:18.
2. Kututia moyo kuendelea kukesha, kuwa na kiasi, na kuwa tayari kwa ajili ya kutokea upesi kwa Yesu Kristo.
a. Neno la mara kwa mara la Yesu kwa wanafunzi wake kukesha na kukaa tayari kwa kutokea kwake (Luka 12:35-40).
4
b. Paulo anasisitiza katika Warumi 13:11-12 kwamba wakati wa mwisho unakaribia upesi, akitaka tuwe na utayari, wenye kiasi na uangalifu.
c. Zaidi ya hayo, Paulo alitangaza kwa Wathesalonike, kama wana wa nuru, kwamba imewapasa kuwa na kiasi, wakikesha kwa ajili ya kuja kwake, 1 Thes. 5:6-9.
d. Petro anawaambia Wakristo wanaoteswa wa Asia Ndogo kuwa na kiasi na kuweka tumaini lao kikamilifu juu ya neema itakayokuja katika ufunuo wa Yesu, 1 Pet. 1:13.
Made with FlippingBook Learn more on our blog