The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide
This is the Swahili edition of Capstone Module 2 Mentor Guide.
Jiwe Walilolikataa Waashi Limekuwa Jiwe Kuu la Pembeni
THE URBAN
Ufalme wa Mungu
MINISTRY INSTITUTE huduma ya WORLD IMPACT, INC.
Mwongozo wa Mkufunzi
Moduli ya 2 Theolojia & Maadili
SWAHILI
MWONGOZO WA MKUFUNZI
Ufalme wa Mungu
Moduli ya 2
Theolojia na Maadili
Kupingwa kwa Utawala wa Mungu
Kuzinduliwa kwa Utawala wa Mungu
Uvamizi wa Utawala wa Mungu
Kukamilika kwa Utawala wa Mungu
Mtaala huu ni matokeo ya maelfu ya masaa ya kazi iliyofanywa na taasisi ya The Urban Ministry Institute (TUMI) na haupaswi kudurufu bila idhini ya taasisi hiyo. TUMI inatoa idhini kwa yeyote anayehitaji kutumia vitabu hivi kwa ajili ya faida ya ufalme wa Mungu, kwa kutoa leseni za kudurufu za gharama nafuu. Tafadhali thibitisha kwa Mkufunzi wako ikiwa kitabu hiki kimepewa leseni ipasavyo. Kwa taarifa zaidi kuhusu TUMI na taratibu zetu za utoaji leseni, tembelea www.tumi.org na www.tumi.org/license .
Moduli ya 2 ya Mtaala wa Capstone: Ufalme wa Mungu – Mwongozo wa Mkufunzi ISBN: 978-1-62932-371-8 © 2005, 2011, 2013, 2015. The Urban Ministry Institute. Haki Zote Zimehifadhiwa. Toleo la kwanza 2005, Toleo la pili 2011, Toleo la tatu 2013, Toleo la nne 2015. © 2017 Kiswahili. Kimetafsiriwa na Samuel Gripper na Eresh Tchakubuta Tunatambua na kuheshimu utumishi uliotukuka wa Mtume K. E. Kisart kwa kujitolea kwake bila kukatishwa tamaa kuwafundisha viongozi katika Injili. Hairuhusiwi kunakili, kusambaza na/au kuuza vitabu hivi, au matumizi mengine yoyote pasipo idhini, isipokuwa kwa matumizi yanayo ruhusiwa kwa mujibu wa sheria ya Haki Miliki ya Mwaka 1976 au kwa idhini ya maandishi kutoka kwa mmiliki. Maombi ya idhini yatumwe katika maandishi kwa taasisi ya: The Urban Ministry Institute, 3701 E. 13th Street, Wichita, KS 67208. The Urban Ministry Institute ni huduma ya World Impact, Inc. Nukuu zote za Maandiko, isipokuwa kama imeonyeshwa vinginevyo, zimechukuliwa kutoka katika SWAHILI BIBLE UV050(MCR) series® Haki Miliki © 1997, iliyochapishwa na The Bible Society of Tanzania. Imetumiwa kwa ruhusa. Haki zote za kimataifa zimehifadhiwa.
Yaliyomo
Muhtasari wa Kozi
3 5 7
Kuhusu Mkufunzi
Utangulizi wa Moduli
Mahitaji ya Kozi
15
Somo la 1 Kupingwa kwa Utawala wa Mungu
1
41
Somo la 2 Kuzinduliwa kwa Utawala wa Mungu
2
69
Somo la 3 Uvamizi wa Utawala wa Mungu
3
97
Somo la 4 Kukamilishwa kwa Utawala wa Mungu
4
137
Viambatisho
297
Kufundisha Mtaala wa Capstone
307
Maelekezo kwa Mkufunzi – Somo la 1
319
Maelekezo kwa Mkufunzi – Somo la 2
329
Maelekezo kwa Mkufunzi – Somo la 3
341
Maelekezo kwa Mkufunzi – Somo la 4
/ 3
UFALME WA MUNGU
Kuhusu Mkufunzi
Mchungaji Dkt. Don L. Davis ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya The Urban Ministry Institute na ni Makamu wa kwanza wa Rais wa World Impact. Alisoma katika Chuo cha Wheaton College na Chuo cha Uzamili cha Wheaton na kuhitimu kwa ufaulu wa kiwango cha juu, yaani Summa Cum Claude, katika ngazi ya Shahada (1988) na Shahada ya Uzamili (1989) katika Masomo ya Biblia na Theolojia ya Utaratibu. Alipata Shahada yake ya Uzamivu katika Masuala ya Dini (Theolojia na Maadili) katika chuo kikuu cha Iowa School of Religion. Akiwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi na Makamu wa Rais Mwandamizi wa World Impact , anasimamia mafunzo ya wamishenari wa mijini, wapanda makanisa, na wachungaji wa majiji, na kufanya uwezeshaji kupitia fursa za mafunzo kwa watendakazi Wakristo wa mijini katika uinjilisti, ukuaji wa kanisa, na umisheni wa upainia. Pia anaongoza Mpango wa Mafunzo huria kwa wale wanaosoma wakiwa mbali, vilevile anawezesha Mafunzo ya Kiuongozi kwa mashirika na madhehebu kadhaa kama Prison fellowship, The Evangelical Free Church of America na The Church of God in Christ. Dkt. Davis, ambaye ametunukiwa tuzo nyingi za ualimu na za kitaalamu, amewahi kuwa profesa na Mkuu wa vitivo katika taasisi kadhaa za kitaalamu zenye hadhi ya juu, baada ya kuhadhiri na kufundisha kozi za dini, theolojia, falsafa, na mafunzo ya Biblia katika taasisi za elimu ya juu kama vile Chuo cha Wheaton, Chuo Kikuu cha St. Ambrose, Programu ya Shahada ya Uzamili ya Theolojia ya Chuo Kikuu cha Houston, Kitengo cha Dini cha Chuo Kikuu cha Iowa, na Taasisi ya Mafunzo ya Ibada ya Robert E. Webber. Ameandika idadi kubwa ya vitabu, mitaala, na nyenzo za kujifunzia ili kuwaandaa viongozi wa mijini, ikijumuisha mtaala wa mafunzo wa Capstone (hii ni programu mama ya TUMI yenye moduli 16 za hadhi ya mafunzo ya seminari, yanayotolewa kupitia mfumo wa elimu ya masafa), Mizizi Mitakatifu: Kidokezo cha Namna ya Kurejesha Mapokeo Makuu , ambayo inaangazia namna makanisa ya mijini yanavyoweza kufanywa upya kupitia kugundua upya imani halisi, sahihi ya kihistoria; na Mweusi na Mwanadamu: Kumgundua Upya M.L. King kama Nyenzo ya Theolojia na Maadili ya Weusi . Dkt. Davis pia ameshiriki katika mihadhara ya kitaalamu kama the Staley Lecture series, makongamano ya kufanywa upya kama Promise Keeper Rallies na miungano ya kithiologia kama The University of Virginia Lived Theology Project Series. Vilevile alipokea tuzo ya heshima ya mwanafunzi mashuhuri ( Alumni Fellow Award ) kutoka Chuo Kikuu cha Iowa cha Sanaa na Sayansi za Kiliberali mnamo 2009. Dkt. Davis pia ni mwanachama wa The Society of Biblical Literature, na The American Academy of Religion .
/ 5
UFALME WA MUNGU
Utangulizi wa Moduli
Salamu, wapendwa marafiki, katika Jina lenye nguvu la Yesu Kristo! Kati ya mambo yote yaliyohubiriwa na kufundishwa na Yesu wa Nazareti, hakuna somo lolote lililo muhimu na lenye kubishaniwa kama habari ya Ufalme wa Mungu. Wasomi wote wa kihafidhina na wasomi huru wanakubali kwamba somo alilopenda zaidi Yesu, ambalo alihubiri na kufundisha mara nyingi zaidi, ni Ufalme wa Mungu. Lilikuwa ni ujumbe wake wa wokovu, mpango wake mkuu, na theolojia yake pendwa na ya moyo wote. Cha kusikitisha ni kwamba, Kanisa la kisasa linaonekana kutozingatia sana kile ambacho Yesu alikiona kuwa muhimu zaidi katika huduma yake ya kinabii na ya Kimasihi. Tumaini letu ni kwamba moyo wako utashikwa na hadithi ya ufalme – Mfalme na Ufalme wake – na kuona umuhimu wake katika maisha ya ufuasi wa kibinafsi na huduma. Somo la kwanza, Kupingwa kwa Utawala wa Mungu , linalenga juu ya Mungu kama Mkuu na Mwenye Enzi. Somo hili linazungumzia jinsi enzi kuu na ubwana kamili wa Mungu ulivyopuuzwa na ibilisi na malaika zake, na wanadamu wawili wa kwanza, Adamu na Hawa, kupitia kutotii kwao kimakusudi katika bustani. Uasi huu ulileta matokeo ya kusikitisha ulimwenguni, katika asili ya mwanadamu, na ukasababisha kuenea kwa milki ya giza ulimwenguni. Hata hivyo, licha ya uasi wetu, Mungu anakusudia kurejesha mbingu na nchi chini ya utawala wake, na kuumba upya ulimwengu ambamo jina lake litatukuzwa, na haki na amani yake vitatawala milele. Katika somo letu la pili, Kuzinduliwa kwa Utawala wa Mungu , tutachunguza nia ya Mungu ya kuondoa uasi na ukaidi wote ambao ni matokeo ya Anguko – Mungu anakuwa Shujaa katika ulimwengu huu ulioanguka. Mungu alifanya agano na Abramu kama ahadi yake ya dhati ya kumleta Mzao ambaye kupitia kwake ufalme na utawala wa shalom na haki ungerejea duniani. Ahadi hii ya agano ilifanywa upya kwa Isaka na Yakobo, kwa taifa la Israeli, kwa kabila la Yuda, na hatimaye kwa familia ya Daudi. Hapa tunafuatilia kwa karibu asili ya Masihi, ambaye kupitia Yeye utawala wa Mungu unarudi katika ulimwengu huu ulioanguka na uliolaaniwa kwa sababu ya dhambi. Yesu wa Nazareti ni utimilifu wa uwepo wa Ufalme, huku utawala wa Mungu ukidhihirishwa katika kuvaa kwake mwili (umwilisho), kifo, ufufuo, na kupaa kwake. Somo la tatu na la nne linahusu Uvamizi wa Utawala wa Mungu na Kukamilishwa kwa Utawala wa Mungu mtawalia. Sasa kwa kuwa Bwana wetu Yesu alikufa, akafufuka, na kupaa mbinguni, Ufalme wa Mungu unatangazwa katika ulimwengu wote na
6 /
UFALME WA MUNGU
Kanisa lake. Kanisa la Yesu Kristo ni kituo cha—mahali pa au muktadha wa— wokovu wa Mungu, ni mahala pa uwepo unaotia nguvu wa Roho Mtakatifu, kituo cha shalom halisi ya ufalme, mahali ambapo uwepo na nguvu za Mungu zinadhihirishwa kwa uhuru. Utawala wa ufalme wa Mungu utakamilika katika Ujio wa Pili wa Yesu, ambapo kifo, magonjwa, na uovu wote vitawekwa chini, mbingu zote na dunia zitafanywa upya, na Mungu atakuwa Yote katika yote. Hadithi ya Ufalme ni hadithi ya Yesu, na nia ya Mungu ni kurejesha ulimwengu chini ya utawala wake kwa njia ya Kristo. Ombi letu ni kwamba upendo na utumishi wako kwake uongezeke kwa wingi unapojifunza Neno la Mungu kuhusu utawala wa milele wa Mungu! Tunamsifu Mungu kwa hadithi yake ya ufalme, na kwa ajili ya shauku yako kama mwanafunzi wa Neno lake Takatifu!
- Mchungaji Dkt. Don. L. Davis
/ 7
UFALME WA MUNGU
Mahitaji ya Kozi
• Biblia (kwa madhumuni ya kozi hii, Biblia yako inapaswa kuwa tafsiri [mf. BHN, SUV, NEN, SRUV, au NIV, NASB, RSV, KJV, NKJV, n.k. ikiwa utatumia Biblia ya Kiingereza], na sio Biblia iliyofafanuliwa [mf. The Living Lible, The Message ]). • Kila moduli katika Mtaala wa Capstone imeainisha vitabu vya kiada ambavyo vinatakiwa visomwe na kujadiliwa katika muda wote wa kujifunza moduli husika. Tunakuhimiza kusoma, kutafakari, na kufanya kazi husika pamoja na wakufunzi wako, wasimamizi, na wanafunzi wenzako. Kutokana na uhaba wa vitabu unaoweza kujitokeza kwa sababu kadha wa kadha (k.m., kushindwa kuchapisha vitabu vya kutosha), tunaweka orodha yetu ya vitabu rasmi vya Capstone vinavyohitajika kwenye tovuti yetu. Tafadhali tembelea www.tumi.org/books ili kupata orodha ya vitabu vinavyohitajika kwa ajili ya moduli hii. • Daftari na kalamu kwa ajili ya kuchukua maelezo na kufanyia kazi za darasani. • Beasley-Murray, G. R. Jesus and the Kingdom of God . Grand Rapids: Eerdmans, 1986. • Ladd, George Eldon. Crucial Questions about the Kingdom of God . Grand Rapids: Eerdmans, 1952. • ------. The Presence of the Future . Grand Rapids: Eerdmans, 1974. • Snyder, Howard A. The Community of the King . Downers Grove: InterVarsity Press, 1977.
Vitabu na nyenzo zingine zinazohitajika
Vitabu vya kusoma
8 /
UFALME WA MUNGU
Muhtasari wa Mfumo wa Kutunuku Matokeo na Uzito wa Gredi
Mahitaji ya Kozi
Mahudhurio na Ushiriki Darasani . . . . . . ....... 30% Majaribio . . . . . . . . . . . . . . . . ................. 10% Kukariri Maandiko. . . . . . . . . . . . . ............. 15% Kazi za Ufafanuzi wa Maandiko. . . . . . . ........ 15% Kazi za Huduma. . . . . . . . . . . . . .............. 10% Usomaji na Kazi za Kufanyia Nyumbani. . . . .... 10% Mtihani wa Mwisho. . . . . . . . . . . . ............. 10%
alama 90 alama 30 alama 45 alama 45 alama 30 alama 30
alama 30 Jumla: 100% alama 300
Mambo ya Kuzingatia katika Utoaji Maksi
Kuhudhuria kila kipindi ni moja ya masharti ya msingi ya kozi hizi. Kukosa kipindi kutaathiri matokeo yako. Ikiwa una dharura isiyoepukika itakayokulazimu kukosa kipindi, tafadhali mjulishe mkufunzi wako mapema. Ukikosa kipindi ni jukumu lako kutafuta taarifa kuhusu kazi na mazoezi yaliyotolewa, na kuongea na mkufunzi wako pale inapobidi kufanya na kukabidhi kazi kwa kuchelewa. Sehemu kubwa ya mafunzo yanayohusiana na kozi hii hufanyika kupitia mijadala. Kwa sababu hiyo, unahimizwa na kutarajiwa kushiriki kikamilifu katika kila kipindi cha kozi hii. Kila kipindi kitaanza na jaribio fupi kuhusu mawazo ya msingi yaliyofundishwa katika somo lililopita. Njia nzuri zaidi ya kujiandaa na majaribio haya ni kupitia Kitabu cha Mwanafunzi na daftari uliloandikia maelezo ya somo hilo lililopita. Kukariri Neno la Mungu ni kipaumbele cha msingi kwa maisha na huduma yako kama mwamini na kiongozi katika Kanisa la Yesu Kristo. Kozi hii ina mistari ya Biblia michache, lakini yenye umuhimu mkubwa katika jumbe zake. Katika kila kipindi utahitajika kukariri na kunukuu (kwa mdomo au kuandika) mistari ya Biblia uliyopewa na mkufunzi wako. Neno la Mungu ni zana yenye nguvu ambayo Mungu anaitumia ili kuwaandaa watumishi wake kwa kila kazi ya huduma aliyowaitia (2 Tim. 3:16-17). Ili kutimiza matakwa ya kozi hii, lazima uchague kifungu cha Biblia na kufanya uchambuzi wa kina (yaani, eksejesia au ufafanuzi wa Maandiko). Kazi yako iwe na kurasa tano (ziliyochapwa kwa kuacha nafasi mbili kati ya mistari au kuandikwa vizuri kwa mkono), na kushughulikia mojawapo ya vipengele vinne vya Ufalme wa Mungu vinavyozungumziwa katika masomo manne ya kozi hii. Ni shauku na matumaini yetu kwamba utashawishika kikamilifu na kuamini juu ya uwezo wa Maandiko
Mahudhurio na Ushiriki Darasani
Majaribio
Kukariri Maandiko
Kazi za ufafanuzi wa Maandiko
/ 9
UFALME WA MUNGU
kuleta badiliko na athari chanya katika maisha yako na ya wale unaowahudumia. Unapoendelea kujifunza kozi hii, uwe huru kuongeza mistari kadhaa katika uchambuzi wako (takriban mistari 4-9) kuhusu jambo ambalo ungependa kujifunza kwa kina. Maelezo yote kuhusiana na kazi hii yametolewa katika ukurasa wa 10-11, na yatajadiliwa katika sehemu ya utangulizi ya kozi hii. Matarajio yetu ni kwamba wanafunzi wote watatumia mafunzo haya kivitendo katika maisha yao na katika majukumu yao ya kihuduma. Mwanafunzi atakuwa na jukumu la kufikiria namna ya kufanya mafunzo ya huduma kwa vitendo kwa kutumia kanuni alizojifunza katika mazingira halisi ya huduma. Maelezo ya namna ya kufanya mafunzo kwa vitendo yanapatika katika ukurasa wa 12, na yatajadiliwa katika kipindi cha utangulizi wa kozi. Mkufunzi wako anaweza kutoa kazi za darasani na kazi za nyumbani za aina mbalimbali wakati wa vipindi vya masomo au anaweza kuziandika katika Kitabu cha Mwanafunzi ulichonacho. Ikiwa una swali lolote kuhusu kile kinachohitajika kuhusiana na kazi hizi au muda wa kuzikusanya, tafadhali muulize mkufunzi wako. Ni muhimu kwa kila mwanafunzi kusoma maeneo yote ambayo inampasa kusoma katika vitabu husika vya kozi hii au katika Maandiko Matakatifu ili kujiandaa kwa ajili ya mijadala darasani. Tafadhali hakikisha unajaza na kukabidhi kwa Mkufunzi wako “Fomu ya Ripoti ya Usomeaji” iliyomo katika Kitabu cha Mwanafunzi, kila wiki. Kutakuwa pia na fursa ya kupata alama za ziada endapo utasoma zaidi ya ulivyoagizwa. Mwishoni mwa kozi, Mkufunzi wako atakupa mtihani wa mwisho utakaofanyia nyumbani. Katika mtihani huu hautaruhusiwa kutumia vitabu vyako vya kozi hii isipokuwa Biblia. Utaulizwa swali ambalo litakusaidia kutafakari juu ya yale uliyojifunza katika kozi na namna yanavyoathiri mfumo wako wa fikra na utendaji wako katika huduma. Utakapokabidhiwa mtihani wa mwisho, mkufunzi wako atakupa taarifa zaidi kuhusu tarehe za kukamilisha na kukabidhi mtihani wako na kazi nyinginezo.
Kazi za Huduma
Kazi za Darasani na za Nyumbani
Kazi za Usomaji
Mtihani wa Mwisho wa Kufanyia Nyumbani
Gredi za Ufaulu
Mwishoni mwa kozi hii, gredi zifuatazo zitatolewa na kuhifadhiwa kwenye mbukumbu za kila mwanafunzi: A – Bora D – Inaridhisha B – Nzuri sana F – Hairidhishi (Feli) C – Nzuri I – Isiyokamilika
1 0 /
UFALME WA MUNGU
Matokeo ya mwisho wa kozi yatatolewa katika mfumo wa gredi kwa kutumia skeli ya kutunuku matokeo kwa mtindo wa herufi zenye alama chanya na hasi, kisha alama za gedi yako ya ufaulu katika kazi mbali mbali zitajumlishwa na kugawanywa kwa idadi ya kazi na vipimo vingine husika ili kupata wastani wa matokeo yako ya mwisho. Kuchelewesha au kushindwa kabisa kukabidhi kazi zako kutaweza kuathiri matokeo yako. Hivyo, ni vyema kupangilia shughuli na muda wako mapema na kuwasiliana na mkufunzi wako endapo kutakuwa na changamoto yoyote. Kama sehemu ya ushiriki wako katika moduli ya Ufalme wa Mungu , utahitajika kufanya ufafanuzi (uchambuzi wa kina) wa mojawapo ya vifungu vifuatavyo vya Neno la Mungu: Mathayo 12:22-30 Marko 10:17-27 Luka 4:16-21 Luka 11:15-23 Luka 18:15-17 Isaya 11:1-9 Kusudi la kazi hii ya ufafanuzi ni kukupa fursa ya kufanya uchunguzi wa kina wa kifungu kimoja muhimu juu ya asili na kazi ya Neno la Mungu. Unaposoma mojawapo ya vifungu vilivyopo hapo juu (au andiko ambalo wewe na Mshauri wako mtakubaliana ambalo linaweza kuwa halipo kwenye orodha), imani yetu ni kwamba utaweza kuonyesha jinsi kifungu hiki kinavyoangazia au kuweka wazi umuhimu wa Neno la Mungu kwa maisha yetu ya kiroho na katika maisha yetu pamoja katika Kanisa. Pia tunatamani kwamba Roho akupe utambuzi wa jinsi unavyoweza kuhusianisha maana ya andiko hilo moja kwa moja na mwenendo wako binafsi wa ufuasi, pamoja na jukumu la uongozi ambalo Mungu amekupa kwa sasa katika kanisa na huduma yako. Hii ni kazi ya kujifunza Biblia, na ili kufanya kazi ya eksejesia , ni lazima udhamirie kuelewa maana ya andiko husika katika muktadha wake. Ukishajua andiko lilimaanisha nini kwa wasomaji wake wa kwanza, unaweza kupata kanuni zinazotuhusu sisi sote leo, na kuzihusianisha kanuni hizo na maisha. Mchakato wa hatua tatu rahisi unaweza kukuongoza katika jitihada zako binafsi za kujifunza kifungu cha Biblia: 1. Je, Mungu alikuwa akisema nini kwa watu katika muktadha wa asili wa andiko husika ? Kazi ya Ufafanuzi wa Maandiko (Eksejesia)
Dhumuni
Mpangilio na Muundo
/ 1 1
UFALME WA MUNGU
2. Ni kanuni gani ambazo andiko hili linafundisha ambazo ni kweli kwa watu wote kila mahali, ikiwa ni pamoja na sisi leo ? 3. Ni kitu gani Roho Mtakatifu ananiagiza kufanya kupitia kanuni hii, leo, katika maisha na huduma yangu ? Baada ya kuwa umeyajibu maswali haya katika kujifunza kwako kibinafsi, hapo sasa utakuwa tayari kuendelea kuandika ulichokigundua katika kazi uliyopewa . Angali hapa chini mfano wa muhtasari wa kazi yako: 1. Eleza kile unachoamini kuwa ndio mada kuu au wazo kuu la andiko ulilochagua. 2. Eleza kwa muhtasari maana ya andiko hilo (unaweza kufanya hivi katika aya mbili au tatu, au, ukipenda, kwa kuandika ufafanuzi mfupi wa mstari kwa mstari juu ya kifungu husika). 3. Eleza kanuni kuu moja hadi tatu au maarifa ambayo kifungu hiki kinatoa kuhusu Neno la Mungu. 4. Eleza jinsi kanuni moja, kadhaa, au zote zinaweza kuhusiana na yafuatayo: Kwa msaada au mwongozo, tafadhali uwe huru kusoma vitabu vya rejea vya kozi hii na/au vitabu vya mafafanuzi ( commentaries ), na kutumia maarifa yaliyomo katika vyanzo hivyo katika kazi yako. Unapotumia maarifa au mawazo ya mtu mwingine kujenga hoja zako, hakikisha unatambua kazi za waandishi husika kwa kutaja vyanzo vya taarifa hizo. Astahiliye heshima apewe heshima yake. Tumia marejeleo ya ndani ya maandishi ( in-text-refences ), tanbihi ( footnotes ), au maelezo ya mwisho ( endnotes ). Njia yoyote utakayochagua kutaja rejea zako itakubalika, ilimradi 1) utumie njia hiyo moja katika kazi nzima, na 2) uonyeshe pale unatumia mawazo ya mtu mwingine, na umtambue mwandishi husika kwa kumtaja. (Kwa maelezo zaidi, angalia katika Kiambatisho cha Namna ya Kuandika Kazi Yako: Mwongozo wa Kukusaidia Kutambua Waandishi wa Vitabu vya Rejea ). Kabla hujakabidhi kazi yako, hakikisha inasifa zifuatazo: • Imeandikwa au kuchapwa vizuri na inasomeka na kueleweka. a. Kiroho chako binafsi na namna unavyotembea na Kristo b. Maisha na huduma yako katika kanisa lako la mahali pamoja c. Hali au changamoto katika jamii yako kwa ujumla.
• Ni uchambuzi wa mojawapo ya vifungu hapo juu. • Imekusanywa kwa wakati (haijacheleweshwa).
1 2 /
UFALME WA MUNGU
• Ina urefu wa kurasa 5. • Inafuata muhtasari au mpangilio uliotolewa hapo juu, na imeandikwa kwa namna ambayo msomaji ataweza kuelewa. • Inaonyesha jinsi kifungu husika kinavyohusiana na maisha na huduma leo. Usiruhusu maagizo haya yakuogopeshe; hii ni kazi ya kujifunza Biblia! Unachohitaji kuonyesha katika kazi hii ni kwamba ulisoma andiko husika, umeeleza kwa muhtasari maana yake, ukaweza kupata kanuni chache muhimu kutoka katika andiko hilo, na kuzihusianisha na maisha na huduma yako mwenyewe. Kazi ya ufafanuzi inabeba alama 45 na inawakilisha 15% ya jumla ya maksi zako, hivyo hakikisha kwamba unaifanya kazi yako kuwa bora na yenye maarifa ya kutosha ya Neno la Mungu. Uongozi wa Kikristo sio tu kujua kile ambacho Biblia inasema; unahusisha uwezo wa kutumia Neno la Mungu kwa njia ambayo wengine wanajengwa na kukamilishwa kwa ajili ya kazi ya huduma. Neno la Mungu ni hai na linafanya kazi, na hupenya hadi kwenye kiini cha maisha yetu na mawazo ya ndani kabisa (Ebr. 4:12). Mtume Yakobo anaweka msisitizo zaidi juu ya kuwa watendaji wa Neno la Mungu, sio wasikiaji tu, tukijidanganya wenyewe. Tunahimizwa kulifanyia kazi, kulitii. Anaongeza kusema kwamba kupuuza nidhamu hii ni sawa na sisi kujitazama sura zetu za asili katika kioo na mara tunapoondoka tunasahau asili yetu (sis ni nani) na tulichokusudiwa kuwa. Katika kila hali, mtendaji wa Neno la Mungu atabarikiwa katika kila atendalo (Yak. 1:22-25). Shauku yetu ya dhati ni kwamba uweze kutumia maarifa unayojifunza kwa vitendo, ukiihusianisha elimu hii na masuala na mahitaji halisi katika maisha yako binafsi, na huduma yako ndani ya kanisa lako na kupitia kanisa lako. Kwa hivyo, sehemu hii muhimu ya kukamilisha moduli hii itakuhitaji kubuni kazi ya huduma kwa vitendo ili kukusaidia kushirikisha wengine baadhi ya maarifa ambayo umejifunza katika kozi hii. Kuna njia nyingi ambazo unaweza kutumia kutimiza takwa hili la kujifunza kwako. Unaweza kuchagua kuwa na muda wa kujifunza na mtu binafsi, kutumia madarasa ya Shule ya Jumapili, vikundi vya vijana au watu wazima, au hata kwa kupata nafasi ya kuhudumu mahali fulani. Unachotakiwa kufanya ni kuhakikisha unajadili na hadhira baadhi ya maarifa uliyojifunza kutoka darasani. (Bila shaka, unaweza kuchagua kuwashirikisha baadhi ya maarifa toka katika kazi yako ya Ufafanuzi wa Maandiko ya moduli hii). Kazi ya Huduma
Utoaji Maksi
Dhumuni
Mpangilio na Muundo
/ 1 3
UFALME WA MUNGU
Uwe huru na tayari kubadilika na kuendana na mazingira yoyote unapofanya kazi yako. Ifanye iwe yenye ubunifu na inayoruhusu kusikiliza mitazamo tofauti kwa nia ya kujifunza. Fanya uchaguzi mapema kabisa kuhusu aina ya muktadha ambao unatamani kutumia kushirikisha watu wengine maarifa haya na kisha mshirikishe Mkufunzi wako juu ya maamuzi hayo. Panga hayo yote mapema na epuka kusubiri dakika za mwisho kuamua na kutekeleza kile unachotaka katika kazi yako. Baada ya kutekeleza kazi yako, andika kwa ufupi (ukurasa mmoja) tathmini ya kazi yako na umkabidhi mkufunzi wako. Mfano wa muhtasari wa Kazi ya Huduma ni kama ifuatavyo: 1. Jina lako 2. Eneo ulilolitumia na hadhira uliyowashirikisha. 3. Muhtasari wa namna muda wako ulivyoenda, namna ulivyojisikia na namna watu walivyoitikia. 4. Ulijifunza nini kupitia mchakato mzima wa kazi yako. Kazi ya huduma inabeba alama 30 ambazo zinawakilisha 10% ya jumla ya maksi zako, hivyo hakikisha unashirikisha yale uliyojifunza kwa ujarisi na ripoti yako iwe yenye kueleweka vizuri.
Utoaji maksi
/ 1 5
UFALME WA MUNGU
Kupingwa kwa Utawala wa Mungu
SOMO LA 1
ukurasa 307 1
Karibu katika Jina lenye nguvu la Yesu Kristo! Baada ya kusoma, kujifunza, kushiriki katika mijadala, na kutendea kazi yaliyomo katika somo hili, utakuwa na uwezo wa: • Kueleza jinsi Mungu kama Bwana, anavyotawala juu ya vyote, lakini kwamba utawala wake ulipingwa kupitia uasi wa kishetani huko mbinguni, na kupitia uasi wa hiari na kutotii kwa wenzi wa kwanza wa kibinadamu duniani. • Kuonyesha jinsi uasi huu ulivyosababisha laana juu ya uumbaji, iliyopelekea kifo, na maafa makubwa zaidi ya wanadamu wote, jambo ambalo Kanisa huliita “Anguko.” • Kuonyesha namna ambavyo kutotii huku kwa Shetani na wanadamu wawili wa kwanza kumeleta matokeo yenye kuhuzunisha na ya uharibifu katika nyanja tatu za uhai na maisha katika uumbaji: kosmos (ulimwengu), sarx (mwili wa asili ya mwanadamu), na kakos (ushawishi unaoendelea na machafuko ya yule mwovu). • Kukariri kwa moyo kifungu kinachohusiana na kupingwa kwa utawala wa Mungu. Soma Zaburi 2:1-12. Je, Mungu anacheka? Katika mojawapo ya maandiko ya kustaajabisha zaidi katika Maandiko Matakatifu, tunasoma hapa kuhusu nia ya mataifa ya kupinga utawala wa Bwana na Mpakwa-Mafuta wake. Kwa kuitikia jaribio hili lisilo na maana la mataifa la kujitenga na utawala wa ufalme wa Mungu, mtunga-zaburi anadokeza kwamba Bwana atazicheka jitihada zao ndogo na duni za kupinga utawala wake. Kwa hakika, Bwana anathibitisha kwamba amemweka Mfalme wake juu ya Sayuni, mlima wake mtakatifu, na kwamba Mwanawe atatawala bila kupingwa akiwa Bwana wa wote. Mpakwa-Mafuta wa BWANA atamiliki mataifa hadi miisho ya dunia, na kuyavunja-vunja mataifa hayo yenye upinzani kama mitungi ya udongo. Mtunga-zaburi anamalizia maono haya makuu kwa kusihi wafalme wa dunia wawe na utambuzi na kupokea onyo. Imewapasa kumwabudu BWANA, kama Mfalme juu ya vyote, na kumsujudia Mwana kwa Utawala wa Mpakwa Mafuta wa BWANA
Malengo ya Somo
ukurasa 307 2
1
Ibada
ukurasa 307 3
1 6 /
UFALME WA MUNGU
kumbusu miguu yake, ili ghadhabu na hasira yake isije ikaachiliwa, wakaangamizwa katika ghadhabu yake kuu. Hebu tukubaliane kwa moyo wote na mtunga-zaburi katika mstari wa 12: «Heri wote wanaomkimbilia» (Zab. 2:12).
Baada ya kutamka na/au kuimba Kanuni ya Imani ya Nikea (katika kiambatisho), sali sala ifuatayo: Mungu wa Milele, Baba yetu, tunakushukuru kwamba wewe peke yako ndiwe Mungu, unayetawala juu zaidi ya mbingu na nchi kama Bwana Mungu Mwenye Enzi Kuu. Ijapokuwa utawala wako wa haki ulipingwa na malaika na wanadamu, umerejesha utawala wako kupitia Mwanao, na hivi karibuni utafanya vitu vyote hapa duniani kama vile mbinguni – sawa sawa na mapenzi yako matakatifu na mema. Utukuzwe kupitia sisi tunapoishi kwa kudhihirisha utawala wako wa haki katikati ya watu wako, Kanisa, kama ushuhuda kwa jamii zetu na ulimwengu wetu. Katika jina la Yesu, Amina.
Kanuni ya Imani ya Nikea na Maombi
ukurasa 307 4
1
Hakuna jaribio kwa somo hili
Jaribio
Mazoezi ya Kukariri Maandiko
Hakuna Maandiko ya kukariri katika somo hili
Hakuna kazi za kukusanya katika somo hili
Kazi za Kukusanya
MIFANO YA REJEA
Ulimwengu Ulioshindikana
Hebu fikiria unazungumza na mmoja wa majirani zako kuhusu hali ya sasa ya jamii na ulimwengu. Ungemjibuje jirani yako ikiwa angetoa kauli ifuatayo: “Kutokana na kila kitu ninachoona katika jamii, na kutokana na matukio haya yote katika ulimwengu, nadhani kwamba Mungu, kama kweli yeye ni halisi, basi ni ama hana udhibiti juu ya ulimwengu, au hawezi kukabiliana na kiwango cha uovu uliomo. Kila kitu kinaharibika. Haiwezekani Mungu akawa na udhibiti – ulimwengu umeharibika sana!” Je kauli hii inaendana na mawazo yako? Kwa nini ndiyo au kwa nini hapana? Unawezaje kumjibu mtu ambaye ana maoni ya namna hii kuhusu ulimwengu wetu leo?
1
ukurasa 308 5
/ 1 7
UFALME WA MUNGU
Ushahidi wa Utawala wa Mungu Duniani
Ingawa Biblia inafundisha kwamba Mungu ni Mweza wa Yote, inaonekana kwamba ulimwengu haujui kabisa nguvu na utukufu wake. Toa sababu tano zinazofanya kuwe na mantiki kusema kwamba ingawa ulimwengu unateseka kutokana na ukosefu wa haki, uonevu, na jeuri, Mungu angali ni Mungu Mweza wa Yote, mwenye uwezo na mamlaka yote, na anayedhibiti kila kitu.
2
Ikiwa Kweli Mungu Anatupenda. . .
Pata picha kwamba umeitwa kwenye nyumba ya familia moja pendwa ambayo kijana wao aliuawa hivi majuzi wakati wa tukio la ufyatulianaji wa risasi usio na sababu wa magenge ya uhalifu. Unapokuwa hapo ukisaidia kuifariji familia, mmoja wa wana familia anasema mbele ya wote waliopo, “Ukweli kwamba jambo hili lilitukia unaonyesha kwamba Mungu hatupendi kiukweli. Ikiwa kweli Mungu anatupenda, mambo ya aina hii yasingetokea kamwe. Mungu mwema angewezaje kuruhusu mambo ya aina hii yatendeke kwa kijana mdogo na asiye na hatia?” Je, jibu lako litakuwa nini kwake na kwa wengine waliosikia maoni haya kutokana na mkasa huo?
1
3
Kupingwa kwa Utawala wa Mungu Sehemu ya 1
YALIYOMO
Mch. Dkt. Don. L. Davis
Mungu, kama Bwana, anatawala juu ya vyote, lakini utawala wake ulipingwa kupitia uasi wa kishetani huko mbinguni, na kupitia uasi wa hiari na kutotii kwa wanadamu wawili wa kwanza duniani. Upinzani huu ulisababisha laana juu ya uumbaji, iliyopelekea kifo, na tatizo kubwa zaidi ya maafa yote yanayowakumba wanadamu. Kanisa linaita tatizo hilo “Anguko.” Kusudi letu katika sehemu hii ya kwanza ya Kupingwa kwa Utawala wa Mungu ni kukuwezesha kuona kwamba: • Mungu ndiye Mwenye Enzi Kuu juu ya ulimwengu wote. • Ubwana wake ulipingwa, na ibilisi na malaika zake, na wanadamu wawili wa kwanza, Adamu na Hawa, kupitia kutotii kwao kimakusudi katika bustani.
Muhtasari wa Sehemu ya 1
ukurasa 308 6
1 8 /
UFALME WA MUNGU
• Dhambi katika ulimwengu hutokea kwa njia hii ya kuasi ukuu wa Mungu na utawala wake. • Kusudi la Mungu ni kurejesha mbingu na nchi chini ya utawala wake, na kuumba upya ulimwengu ambamo jina lake litatukuzwa, na haki na amani yake vitatawala milele.
I. Mungu Mwenyezi, Mungu wa Utatu, Ambaye Jina Lake ni YHWH (Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu), ni Bwana wa Wote.
Muhtasari wa Sehemu ya 1 ya Video
1
A. Mungu anajitegemea mwenyewe, ana uhai ndani yake mwenyewe, na anapata uzima wake kutoka katika nafsi yake mwenyewe.
ukurasa 309 7
1. Kutoka 3:14
2. Yohana 5:26
3. Matendo 17:25
B. Bwana Mungu ndiye Muumba na Mmiliki wa vitu vyote.
ukurasa 309 8
1. Ex nihilo
2. Mwanzo 1:1
3. Yeremia 10:10-13
4. Hakika Mungu wa Utatu ndiye Bwana; Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, ambaye anatawala kama Mfalme, na ameumba vitu vyote kwa utukufu wake.
/ 1 9
UFALME WA MUNGU
C. Ukuu wa Mungu umekita mizizi katika nafsi yake, na kudhihirishwa katika kazi zake zote. Dk. Lewis Chafer, mwanzilishi wa Seminari ya Dallas, na Dk. Walvoord, katika kuzungumza juu ya ukuu wa Mungu wanaeleza: . . . sifa za Mungu zinaweka wazi kwamba Mungu ni mkuu juu ya vyote. Hajitiishi chini ya nguvu nyingine, mamlaka nyingine au utukufu mwingine, na hayuko chini ya yeyote kwa kuwa hakuna aliye mkuu kuliko Yeye mwenyewe. Anawakilisha ukamilifu kwa kiwango kisicho na kikomo katika kila kipengele cha uwepo wake. Hawezi kamwe kushangaa, kushindwa, au kutokuwa na uhakika. Hata hivyo, bila kudhabihu mamlaka yake au kuhatarisha utimilifu wa mwisho wa mapenzi yake makamilifu, imempendeza Mungu kuwapa [wanadamu] {watu} kiasi cha uhuru wa kuchagua, na kwa ajili ya utekelezaji wa uchaguzi huo Mungu huwawajibisha [wanadamu] {watu}. Lewis Sperry Chafer na John Walvoord. Major Bible Themes . Grand Rapids: Zondervan, 1975. uk. 42.
ukurasa 310 9
1
1. Danieli 4:34-35
2. Bwana ni Mungu, Mungu mkamilifu asiye na kikomo, ambaye anastahili ibada na utii wetu.
3. Utawala wa Mungu umepingwa.
a. Na adui mkuu wa wanadamu, Ibilisi
b. Na wanandoa wa kwanza wa kibinadamu
II. Uasi wa Ibilisi (Shetani) mbinguni unawakilisha upinzani wa kwanza na mbaya zaidi kwa Enzi Kuu ya Mungu katika Ulimwengu.
ukurasa 310 10
A. Maelezo ya Agano la Kale ya Shetani kama Lusifa, Mwana wa Asubuhi
2 0 /
UFALME WA MUNGU
1. Kiumbe aliyeumbwa, taz. Kol. 1:16
2. Kiumbe binafsi (angalia asili yake katika majaribu ya Yesu, taz. Luka 4:1-13)
B. Kanuni kuu ya uasi wa Shetani na utendaji wa kishetani unaotajwa katika Biblia: upinzani dhidi ya mapenzi ya Mungu kupitia kiburi, kujiinua, na machafuko, Isa. 14:12-17
1
1. Nitapanda mpaka mbinguni.
2. Nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu.
3. Nitaketi juu ya mlima wa mkutano, pande za mwisho za kaskazini.
4. Nitapanda juu kupita vimo vya mawingu.
5. Nitafanana na yeye Aliye juu.
6. Hatima ya shetani: mst. 15-17
7. Nia kuu ya utendaji wa kishetani: “Nitakuwa kama Aliye Juu.”
a. Mwanzo 3: kishawishi cha kukubali falsafa hii
/ 2 1
UFALME WA MUNGU
b. Tabia za uasi
(1) Kujitosheleza (2) Kujitegemea nje ya Mungu
(3) U-mimi (4) Ubinafsi
c. Kiburi cha Shetani ni mwanzo wa uasi katika ulimwengu, na sababu kuu ya dhambi zote na ukosefu wa haki.
1
C. Vita mbinguni: Dhambi ya Shetani na mlolongo wa uasi
1. Kuanguka kwa idadi kubwa ya malaika (yaani mapepo), Ufu. 12
2. Jaribu la watu wawili wa kwanza katika bustani
III. Utawala wa Mungu ulipingwa kupitia kutotii kwa Adamu na Hawa: Anguko, Mwa. 3.
A. Anguko la wanadamu halielezeki.
1. Walifanywa kwa ukamilifu na kwa namna ya ajabu kuwa hawana hatia, na hivyo kuweza kudanganywa.
2. Hali ya wanadamu kabla ya Anguko
a. Waliishi kwa muda usiojulikana katika ushirika na Mungu.
2 2 /
UFALME WA MUNGU
b. Waliishi chini ya baraka na utunzaji wa Mungu.
c. Wakapewa mamlaka juu ya uumbaji, wakiwapa majina viumbe.
d. Walitembea katika ushirika na Mungu katika mazingira makamilifu yasiyo na madhara ya dhambi.
e. Wakiwa wameumbwa bila hatia, waliumbwa kwa mfano wa Mungu, wakiwa na utu kamili, wenye uwezo wa kufanya maamuzi ya kiadili na kufuata miongozo ya Mungu.
1
B. Tukio la Bustani katika Mwanzo 3
1. Angalia shetani: anaelezewaje?
2. Mazungumzo ya nyoka na Hawa, mama wa wote walio hai, kuhusu mti wa uzima
a. Shauku ya nyoka kupinga utawala wa Mungu, Mwa. 3:4-5
b. Mwitikio wa kusikitisha wa mwanamke na mwanamume, Mwanzo 3:6-7
3. Kiini cha udanganyifu wa nyoka: angalia ulinganifu na 1 Yohana 2:16.
a. Aliona wafaa kwa chakula – tamaa ya mwili
/ 2 3
UFALME WA MUNGU
b. Unapendeza kwa macho – tamaa ya macho
c. Una nguvu ya kuleta hekima - kiburi cha uzima
d. Ona uwiano sawa katika jaribu la Yesu, Mt. 4; Marko 1; Luka 4
C. Matokeo ya kutisha ya dhambi ya Adamu na Hawa: ukaidi, mgogoro na aibu, ubinafsi, kutengwa, na hatimaye, kifo.
1
Hitimisho
ukurasa 311 11
» Mungu wa Utatu ndiye Bwana mkuu, anayetawala juu ya vyote.
» Utawala wake ulipingwa kupitia uasi wa kishetani huko mbinguni, na kupitia uasi wa hiari na kutotii kwa wanadamu wawili wa kwanza duniani.
Tafadhali chukua muda mwingi uwezavyo kujibu maswali haya na mengine ambayo yaliibuka kutokana na maudhui ya video. Jibu kwa uwazi na kwa ufupi, na inapowezekana, tumia Maandiko. 1. Biblia inafafanuaje utawala na mamlaka ya Mungu Mweza wa Yote juu ya ulimwengu wote? Ni nini maana ya neno “enzi”? 2. Wanatheolojia wanaposema kwamba Mungu wa Biblia “anajitegemea,” wanamaanisha nini? 3. Kwa nini ni muhimu kwetu kufundisha, kulingana na madai ya Biblia yenyewe, kwamba Mungu aliumba ulimwengu ex nihilo ? 4. Kulingana na Maandiko, enzi kuu na utawala wa Mungu unaenea kwa umbali gani duniani kote, na katika ulimwengu wote? Eleza jibu lako. 5. Unaweza kufafanuaje “kanuni kuu ya uasi wa Shetani” katika ulimwengu? 6. Video ilionyeshaje “nia kuu ya utendaji wa kishetani”? Je, unakubaliana na kauli hii? Kwa nini ndiyo au kwa nini hapana?
Sehemu ya 1
Maswali kwa Wanafunzi na Majibu
ukurasa 311 12
2 4 /
UFALME WA MUNGU
7. Uasi wa Shetani uliathiri nyanja nyingine mbili za uhai katika ulimwengu. Ni zipi, na nini kilitokea kama matokeo? 8. Tunawezaje kuelezea anguko la wanadamu – ni sababu gani tunaweza kutaja zilizopelekea uamuzi wao wa kuasi mamlaka na utawala wa Mungu Mweza wa Yote? 9. Je, jaribu la Shetani kwa Hawa linalinganaje na jinsi Yohana Mtume alivyoeleza kuhusu uovu uliomo ulimwenguni (rej. 1 Yoh. 2:16)? 10. Ni nini kilikuwa matokeo ya kusikitisha ya uasi wa Shetani huko mbinguni, na kutotii kwa Adamu na Hawa katika bustani? Wanatheolojia wanaliitaje tukio hilo baya?
1
Kupingwa kwa Utawala wa Mungu Sehemu ya 2
Mch. Dkt. Don. L. Davis
Kutotii kwa Shetani na wanadamu wawili wa kwanza kumeleta matokeo yenye kuhuzunisha na ya uharibifu katika nyanja tatu za uhai na maisha katika uumbaji: kosmos (ulimwengu), sarx (mwili wa asili ya mwanadamu), na kakos (ushawishi unaoendelea na machafuko ya yule mwovu). Kusudi letu katika sehemu hii ya pili ya somo la Kupingwa kwa Utawala wa Mungu ni kukuwezesha kuona kwamba: • Kutotii kwa Shetani na wanadamu wawili wa kwanza kumeleta matokeo yenye kuhuzunisha na yenye ya uharibifu katika nyanja tatu. • Kosmos inawakilisha muundo wa ulimwengu wa sasa na mfumo wa uasi na dhambi. • Sarx inawakilisha ubinadamu na hali ya dhambi katika asili ya mwanadamu, pamoja na kuhesabiwa hatia na matokeo ya kifo cha kimwili na kiroho. • Kakos inawakilisha kuachiliwa kwa Shetani na pepo wabaya katika nyanja ya ulimwengu na dunia, na udhibiti wake uliofuata na uendeshaji wa maisha na mifumo ya mwanadamu kupitia nguvu za uovu.
Muhtasari wa Sehemu ya 2
ukurasa 311 13
/ 2 5
UFALME WA MUNGU
I. Matokeo ya kwanza ya Anguko, kuibuka kwa kosmos : neno la Kiyunani likimaanisha “muundo huu wa dunia ya sasa na mfumo wa uasi na dhambi.”
Muhtasari wa Sehemu ya 2 ya Video
ukurasa 312 14
A. Anguko limezaa kosmos , mfumo wa sasa wa ulimwengu usiomcha Mungu ambao unafanya kazi kulingana na kanuni za uasi zilizouanzisha.
1. Inafanya kazi chini ya mamlaka ya moja kwa moja ya shetani, chini ya udhibiti wake wa moja kwa moja, Mt. 4:8-10.
1
2. Dunia yote iko chini ya utawala wa yule Mwovu, 1 Yoh. 5:19.
3. Roho Mtakatifu anayekaa ndani ya waamini ni mkuu kuliko yule (Shetani) aliye katika dunia, 1 Yoh. 4:1-4.
B. Shetani, akiwa adui mkuu wa Mungu, anadhibiti mfumo huu wa dunia kupitia pupa, tamaa, na kiburi.
1. Eneo lililojaa uasi, majaribu, na ukosefu wa haki.
2. Mfumo ulio katika mgogoro wa kina, unaoendelea na Mungu.
3. Muundo ambao Mungu mwenyewe siku moja atauhukumu na kuuharibu.
4. Ghadhabu ya Mungu dhidi ya mfumo wa dunia ya sasa, Yakobo 4:4.
C. Falme na mamlaka: miundo na matabaka ya upinzani na dhambi.
ukurasa 313 15
2 6 /
UFALME WA MUNGU
1. Mfumo wa sasa wa dunia uko chini ya utendaji na mwingilio wa falme na mamlaka mbalimbali.
2. Majeshi ya roho za giza yanaathiri na kuendesha mambo ya wanadamu.
3. Angalia upinzani wa majeshi ya roho ovu dhidi ya maombi ya Danieli katika Danieli 9-10.
1
D. Msukumo wa kiroho wa kosmos : tamaa, uchoyo, na kiburi, 1 Yohana 2:15-17
1. Amri kwa wanafunzi: msiipende dunia wala mambo vilivyomo.
a. Angalia mzozo kati ya Mungu na dunia.
b. Wale wanaoipenda dunia hawana upendo wa Mungu ndani yao.
2. Muhtasari kuhusu dunia: kila kilichomo duniani (tamaa ya mwili, tamaa ya macho, na kiburi cha uzima) havitokani na Baba, bali ni vya dunia yenyewe.
3. Mfumo wa dunia unapita, pamoja na tamaa zake.
4. Athari kuu ya kwanza ya uasi katika dunia imekuwa kuzuka kwa mfumo huu wa kidunia wa tamaa, kiburi, na uchoyo.
/ 2 7
UFALME WA MUNGU
II. Matokeo ya pili ya Anguko, Sarx : kupotoshwa na kukengeuka kwa asili ya mwanadamu (kama matokeo ya kosa la Adamu). Mambo manne muhimu kuzingatia kuhusu dhambi:
ukurasa 313 16
A. Dhambi ya kibinafsi: yote yanayofanywa, kufikiriwa, na kusemwa katika maisha yetu ambayo ni kinyume au kushindwa kuendana na tabia ya Mungu.
1. Rum. 3:23.
1
2. Kutofuata tabia na mapenzi ya Mungu katika matendo ambayo tunafanya au tunashindwa kufanya.
3. Dhambi kama chipukizi la kutotii kwa wanadamu wawili wa kwanza waliokataa utawala wa Mungu.
B. Asili ya dhambi: “mwili,” yaani asili ya dhambi ya wanadamu.
1. Rum. 5:19
2. Efe. 2:3
3. Upinzani wa Adamu kwa utawala wa Mungu ulimfanya kuchukua asili potovu na iliyoharibika.
a. Watoto wa Adamu wanashiriki hatia yake na asili yake.
b. Kutotii kwa Adamu kunaonekana sasa katika mapenzi, dhamiri, na akili zetu.
2 8 /
UFALME WA MUNGU
c. Roho Mtakatifu ndani ya mfuasi: uwezo wa kuushinda mwili, Rum. 8:1-4.
C. Kuhesabiwa dhambi na hatia: hatia kama inavyohukumiwa kwa msingi wa dhambi ya Adamu. Jinsi gani? (Taz. Warumi 5:12-18).
1. Rum. 5:12. Dhambi iliingia ulimwenguni kupitia mtu mmoja, na kifo kupitia dhambi.
1
2. Rum. 5:15. Wengi walikufa kwa kosa la mtu mmoja, Adamu.
3. Rum. 5:17. Kwa sababu ya kosa la mtu mmoja, Adamu, kifo kimetawala juu ya wanadamu wote kupitia dhambi yake.
4. Rum. 5:18. Hukumu inahesabiwa juu ya wanadamu wote kupitia kosa la mtu mmoja, Adamu.
5. Kwa hesabu ya Mungu, ulimwengu wote, Wayahudi na Wamataifa, wanahesabika kuwa chini ya dhambi, k.m. Rum. 3:9 na Gal. 3:22.
D. Kifo, kipengele cha nne na cha mwisho cha matokeo ya dhambi.
1. Rum. 6:23.
2. Kifo cha kimwili NA kifo cha kiroho
a. Hakuna ushirika na Mungu,
/ 2 9
UFALME WA MUNGU
b. Kutengwa na kukatiliwa mbali na chanzo cha uzima.
3. Hitaji la ukombozi: Damu iliyomwagika ya Yesu Kristo (Yohana 14:6).
III. Matokeo ya tatu na mabaya zaidi ya Anguko, Kakos : Kuachiliwa kwa Ibilisi na jeshi lake la mapepo katika dunia.
ukurasa 314 17
1
A. Kweli za utangulizi kuhusu yule Mwovu
1. Nguvu binafsi za shetani haziwezi kukadiriwa.
a. Ana nguvu za mauti, Ebr. 2:14.
b. Ana nguvu za magonjwa, kama inavyoonyeshwa katika kisa cha Ayubu, Ayubu 2:7.
c. Uwezo wake wa kupambana na watu wa Mungu, kama vile kumpepeta Petro kama ngano, Luka 22:31.
2. Ibilisi anasaidiwa na mapepo wanaofanya mapenzi yake na kumtumikia.
a. Yeye hana uwezo wala sifa ya kuwa kila mahali, si muweza wa yote, wala si mjuzi wa yote.
b. Kupitia wajumbe wake anaweza kugusa kila sehemu ya dunia.
3 0 /
UFALME WA MUNGU
B. Kakos ni “mkufuru dhidi ya Mungu”: Shetani anafanya kazi kama mhusika wa ibada ya sanamu na uchafu.
1. Tamaa mbaya ya kujifanya kama Aliye Juu
2. Isaya 14:12-14
3. Tamaa za Shetani: nia ya kupewa utukufu na heshima inafaa kwa Mungu peke yake.
1
4. Kazi ya shetani kimsingi ni kukufuru.
a. Anautafuta utukufu wa Mungu kwa ajili yake mwenyewe.
b. Anaitafuta heshima anayostahili Mungu pekee.
5. Je, shauku hii ya ukuu juu ya Mungu inafanyaje kazi?
C. Kakos ni “mdanganyaji wa ulimwengu”: Shetani anafanya kazi kama roho yenye kudanganya kati ya mataifa.
1. Maneno ya Paulo katika 2 Wakorintho 4:3-4.
2. Maneno ya Yesu katika Yohana 8:44.
3. Athari ya uwezo wa shetani kusema uwongo:
/ 3 1
UFALME WA MUNGU
a. Ibilisi ndiye baba (chanzo) wa uwongo wote.
b. Udanganyifu ndio kiini cha shughuli za kishetani.
c. Dini na falsafa zote za uwongo hutokana na utendaji wa kipepo na wa kishetani.
D. Kakos ni “mshitaki wa ndugu”: kazi ya Shetani kama adui wa watu wa Mungu.
1
1. Anatafuta kuwashawishi Wakristo moja kwa moja, lakini anaweza kupingwa kwa ufanisi.
a. Kwa damu ya Mwana-Kondoo, Ufu 12:9-11
b. Kwa silaha za Mungu, Efe. 6:10-18
c. Kwa imani katika Neno la Mungu (yaani ngao ya imani), Efe. 6:16-17
2. Kulinganisha nguvu na ushawishi wa shetani juu ya waliopotea na waliookolewa
a. Kuwaonea na kuwakatisha tamaa waliookoka,
b. Hana uwezo wa kukaa ndani ya waliookoka na kuwashinda, 1 Yoh 2:1-2.
3. Kazi ya shetani ya mashtaka, Ufu. 12:9-11.
3 2 /
UFALME WA MUNGU
4. Dawa ya mashitaka ya shetani: Yesu ndiye mtetezi wetu, 1 Yohana 2:1-2.
Hitimisho
» Mungu Mwenyezi ni Bwana na anatawala juu ya vyote.
» Utawala wa Mungu ulipingwa kupitia uasi wa kishetani huko mbinguni, na kupitia uasi wa hiari na kutotii kwa wanadamu wawili wa kwanza duniani. » Upinzani huo umeleta matokeo ya kusikitisha na ya uharibifu katika nyanja tatu: kosmos (ulimwengu), sarx (mwili wa asili ya mwanadamu), na kakos (ushawishi unaoendelea na machafuko ya yule mwovu).
1
Tafadhali chukua muda mwingi uwezavyo kujibu maswali haya na mengine ambayo yaliibuka kutokana na maudhui ya video. Jibu kwa uwazi na kwa ufupi, na inapowezekana, tumia Maandiko. 1. Matokeo ya kwanza ya Anguko yalikuwa ni kuibuka kwa kosmos . Neno hili la Kiyunani linarejelea nini? 2. Kosmos hufanya kazi chini ya mamlaka na udhibiti wa nani? Kuna uhusiano gani kati ya Roho Mtakatifu (ambaye hukaa ndani ya waumini) na kosmos ? 3. Kulingana na Yohana Mtume, mfumo wa sasa wa kidunia usiomcha Mungu unafanya kazi kupitia mambo gani matatu? Eleza. 4. Je, mtu anayependa kosmos ana uhusiano gani na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo? Kwa nini? 5. Sarx inawakilisha matokeo ya pili ya Anguko. Neno hili linamaanisha nini? 6. Je, ni mambo gani manne kuhusu dhambi yanayohusiana na sarx ambayo sasa yanatokea kwa watu wote kila mahali kwa sababu ya Anguko? 7. Kulingana na video, ni nini «matokeo mabaya zaidi» ya Anguko? Kakos ana nini juu ya wanadamu kuhusiana na kifo, magonjwa, na kuingilia kwake maisha na mambo ya watu wa Mungu? 8. Kulingana na Biblia, ni njia gani tatu ambazo kwazo kakos hupinga utawala wa Mungu? Je, ufahamu huu wa kakos unatusaidiaje kuelewa vyema matatizo ya majiji yetu na vita vya kiroho leo?
Sehemu ya 2
Maswali kwa Wanafunzi na Majibu
ukurasa 314 18
/ 3 3
UFALME WA MUNGU
MUUNGANIKO
Somo hili limeangazia kweli fulani kuu kuhusu utawala wa Mungu, na upinzani wake kupitia uasi wa Shetani na kutotii kwa Adamu na Hawa. ³ Mungu wa Utatu, YHWH (Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu), ndiye Mwenye Enzi Kuu juu ya ulimwengu, anayeishi kwa kujitegemea mwenyewe, ambaye aliumba ulimwengu ex nihilo kwa utukufu wake. ³ Kama Muumba na Mmiliki wa vitu vyote, enzi kuu ya Mungu imekita mizizi ndani yake, na kudhihirishwa katika kazi zake zote katika uumbaji na matendo yake katika historia. ³ Utawala wa Mungu na haki yake ya kumiliki vilipingwa, mwanzoni na kwa kiasi kikubwa zaidi na shetani katika uasi wake huko mbinguni. ³ Kanuni kuu ya uasi wa kishetani ni kiburi; tamaa yake iliyopotoka ya kupokea heshima na utukufu unaomstahili Mungu pekee. ³ Uasi wa Shetani ulisababisha anguko la malaika wengi waliofuata njia yake, pamoja na jaribu, kutotii, na uasi wa hiari wa Adamu na Hawa katika bustani ya Edeni. Uasi huu mbinguni na duniani unajulikana kama “Anguko.” ³ Matokeo ya kwanza ya Anguko yalikuwa ni kuibuka kwa kosmos , mfumo wa sasa wa ulimwengu usiomcha Mungu ambao unafanya kazi kwa nguvu ya uchoyo, tamaa, na kiburi. ³ Matokeo ya pili ya Anguko yalikuwa kutokea kwa sarx , kupotoshwa na kukengeushwa kwa asili ya mwanadamu, na kusababisha matendo ya dhambi ya kibinafsi, kuingia kwa asili ya dhambi kwa wanadamu (yaani “mwili”), wanadamu wote kuhusishwa na dhambi na hatia kupitia kosa la Adamu, na kifo cha kimwili na kiroho. ³ Matokeo ya tatu ya Anguko na yenye uharibifu zaidi yalikuwa kuachiliwa kwa kakos , ibilisi ambaye sasa anatenda kazi ulimwenguni kama mkufuru dhidi ya Mungu, mdanganyaji wa ulimwengu, na mshitaki wa ndugu. Kupitia Yesu Kristo, tunaweza kumshinda kwa Roho Mtakatifu kupitia Damu ya Mwana-kondoo na neno la ushuhuda wetu, (rej. 1 Yoh. 4:4; Ufu. 12:9-11).
Muhtasari wa Dhana Muhimu
ukurasa 314 19
1
3 4 /
UFALME WA MUNGU
Sasa ni wakati wa wewe kushughulikia maswali yako mwenyewe kupitia majadiliano na wenzako darasani. Katika kutafakari kuhusu somo hili na dhana ulizopitia, ni maswali gani hasa yanayokujia akilini? Labda yafuatayo yanaweza kuibua maswali yako mahususi na muhimu. * Unapaswa kuelewaje maana ya Enzi Kuu ya Mungu katika ulimwengu usio wa haki na usiomcha Mungu? * Je, unahisi ni haki na sahihi kwako kwamba Biblia inafundisha kwamba hali yetu ya sasa ni matokeo ya moja kwa moja ya uasi wa kishetani na wa kibinadamu uliofanywa maelfu ya miaka iliyopita? * Ni dhana gani haileti maana kwako kuhusu matokeo ya Anguko? Je, kuna mapungufu katika uelewa wako wa kosmos , sarx na kakos ? * Je, unatatizika hata kidogo na dhana ya utawala wa Mungu kupingwa? Kwa maneno mengine, ikiwa Mungu ni mweza-yote, kwa nini aliruhusu mtu yeyote, hata Shetani, apinge utawala wake? * Je, Mungu anaweza kuwawajibisha wengine kwa makosa ya watu wengine? Kwa kuwa inaonekana kwamba dhambi na kutotii kwao ni matokeo ya yale ambayo Shetani na Adamu walifanya, si yale waliyofanya wenyewe? Je, hii inawezekanaje? * Je, sisi tunaoamini sasa tunatofautiana kwa kiwango gani na wengine wasiomjua Kristo? Je, bado tuko chini ya udhibiti wa shetani, nguvu za dhambi, na majaribu ya ulimwengu? Ni zana gani, ahadi, baraka, na nyenzo gani ambazo Mungu ametupa ili tuishi chini ya utawala wake leo? Leo, makumi ya maelfu ya vijana wanashiriki katika magenge ya uhalifu ambayo yanaharibu mamia ya vitongoji vya miji kote nchini. Wanaume, wanawake, wavulana, na wasichana wengi wasio na hatia wanaishi kwa hofu ya maisha yao kwa sababu ya shughuli na jitihada za magenge hayo, ambayo mengi yanajihusisha na jeuri, ukatili, na uhalifu. Hata hivyo, kwa wengi wa wale wanaoshiriki katika vikundi hivyo, vikundi hivyo ndio familia pekee ambazo wamewahi kujua. Wanapokea upendo mwingi, heshima, na kujali kwingi kati ya washiriki wa magenge husika na familia zao, ingawa wanapata maumivu mengi pamoja. Katika kuangalia hali ya magenge katika mitaa duni ya majiji, je, theolojia uliyosoma wiki hii inatoa tafsiri gani kwa hali hii? Zaidi ya hilo, je, kuna namna ambazo uhalisia huo wa magenge haujafafanuliwa na mada zinazozungumziwa katika somo la “ Kupingwa Magenge katika Mitaa Duni ya Jiji
Kutendea Kazi Somo na Matokeo yake kwa Wanafunzi
ukurasa 315 20
1
MIFANO
1
ukurasa 315 21
/ 3 5
UFALME WA MUNGU
kwa Utawala wa Mungu ”? Ni maarifa gani yanaweza kutusaidia kuelewa vyema zaidi ukweli huu wa hali za miji na majiji?
Mauaji ya Kimbari ya Wayahudi katika Vita vya Pili vya Dunia
Wakati wa Vita vya Pili vya Dunia, zaidi ya Wayahudi milioni sita waliuawa wakati wa vita vya Ulaya. Mamia ya maelfu ya watoto na watoto wachanga wasio na hatia walichinjwa kwa sababu ya kampeni ya kiwendawazimu ya Hitler ya kuwaondoa watu wote wa asili ya Kiyahudi ulimwenguni – wanaume wazee, wanawake, wavulana, wasichana, vijana, watu wa makamo – mtu yeyote wa urithi wa Kiyahudi. Tunawezaje kusema kwamba Mungu ndiye anayetawala wakati mamilioni mengi sana ya watu wasio na hatia wameteswa na kuuawa bila sababu, kama katika mfano huu mbaya wa Wayahudi? Katika kitabu cha Danieli, tunaona mtakatifu huyu mcha Mungu akimwomba Mungu kwa niaba ya wana wa Israeli. Kama unavyokumbuka, watu wa Israeli walikuwa utumwani kwa sababu ya ukosefu wa haki na ibada ya sanamu waliyokuwa wakifanya hapo awali, na, kama matokeo ya adhabu ya Mungu, aliruhusu watu wake wapelekwe utumwani. Katika maombi ya kina ya maombezi (ona Danieli 10), Danieli anamtafuta Mungu baada ya majuma matatu ya maombolezo. Anatembelewa na malaika ambaye anamwambia kwamba haimpasi kuogopa, kwa sababu tangu siku ya kwanza ambayo alikuwa ameweka moyo wake katika kulielewa hili na juu ya kujinyenyekeza mbele za Mungu maneno yake yalisikiwa, na kwamba yeye, malaika, alikuja kwa ajili ya kuleta majibu ya maombi ya Danieli. Hata hivyo, “mkuu wa ufalme wa Uajemi alinipinga siku ishirini na moja; bali, tazama, huyo Mikaeli, mmoja wa hao wakuu wa mbele, akaja kunisaidia; nami nikamwacha huko pamoja na wafalme wa Uajemi” (ona Danieli 10:12-14). Wengi wanaamini kwamba hii ni dondoo kuhusu aina ya vita vya kiroho vinavyotuzunguka, visivyoonekana lakini vyenye nguvu na halisi. Je, una maoni gani kuhusu mfano huu muhimu lakini wenye utata? Je, kifungu kama hiki kinasaidia au kuzuiaje uelewa wetu wa kupingwa kwa utawala wa Mungu leo? Upinzani kwa Maombi ya Danieli katika Danieli 9-10
2
1
3
Mungu, kama Bwana, anatawala juu ya vyote, lakini utawala wake ulipingwa kupitia uasi wa kishetani huko mbinguni, na kupitia uasi wa hiari na kutotii kwa wanadamu wawili wa kwanza duniani. Upinzani huu, unaojulikana kitheolojia kama “Anguko,” umesababisha laana juu ya uumbaji, na kusababisha uharibifu
Marudio ya Tasnifu ya Somo
Made with FlippingBook Learn more on our blog