The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide

1 0 4 /

UFALME WA MUNGU

(2) Kifo cha pili, kinachozungumziwa katika Ufunuo 21:8, ni kifo cha milele ambacho kinawakilisha, kwa yule ambaye amepotea milele, kutengwa kwake na Mungu milele. (3) Hiki ni tofauti na kinakuja baada ya kifo cha kimwili.

3. Kifo cha kimwili na kiroho ni matokeo ya dhambi, Rum. 6:23; Efe. 2:1-2.

4. Kile kinachoitwa “kifo cha pili,” (kutenganishwa kwa milele kwa mwanadamu na uwepo wa Mungu) hakihusiani na waamini.

a. Kwa wale waliochaguliwa kuingia katika Ufalme wa Kristo, kifo cha pili hakina nguvu (Ufu. 20:6).

b. Kwa kuwa Yesu ndiye ufufuo na uzima, wale wanaomwamini hawatakufa katika mauti ya pili (Yohana 11:25-26).

4

5. Kazi kuu ya ufalme wa Yesu inashinda nguvu ya kifo kwa mwamini.

a. Kupitia kuja kwake duniani ili kumshinda shetani.

b. Kupitia ushindi wake dhidi ya laana.

c. Kupitia malipo yake kwa ajili ya adhabu ya dhambi zetu msalabani kwa damu yake iliyomwagika.

d. Kwa sababu ya haya, hakuna yeyote anayemwamini atakayepitia kifo cha pili au kutengwa na Bwana milele.

Made with FlippingBook Learn more on our blog