The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide
/ 1 0 7
UFALME WA MUNGU
d. Picha ya usingizi imetumika mara tatu katika 1 Wathesalonike 4:13-15.
e. Kulala kwa nafsi ni mtazamo unaochukua taswira hii kiuhalisia kuhusu hali ya nafsi baada ya kifo na kabla ya ufufuo.
3. Je, mtazamo huu unashawishi? Ni mtazamo rahisi, lakini una matatizo makubwa.
a. Biblia huelekea kudokeza kwamba nafsi huendelea kuishi baada ya kifo, na kwamba sisi si tu sehemu moja iliyounganishwa (mwili nafsi-roho), bali kwamba nafsi na mwili ni tofauti.
b. Biblia inafundisha katika sehemu kadhaa kuhusu kuwepo kwa ufahamu wa kibinafsi baada ya kifo. (1) Tajiri na Lazaro, Luka 16:19-31. (2) Neno la Yesu kwa mwizi msalabani, “Amin, nakuambia, leo hivi utakuwa pamoja nami katika Paradiso,” Lk 23:43. (3) Tendo la Yesu mwenyewe kukabidhi roho yake kwa Mungu, Luka 23:46. (4) Paulo anatamani kuondoka na kuwa pamoja na Kristo, ambayo inaashiria ushirika hai na wa kiufahamu na Yesu baada ya kifo, Flp. 1:23.
4
c. Ni lazima tuchukulie kwa uzito maandiko yanayodokeza kwamba kutokuwepo katika mwili ni kuwapo pamoja na Bwana, yaani, katika ushirika wa ufahamu pamoja naye, 2 Kor. 5:8.
C. Hali ya wafu kama toharani.
1. Muhtasari wa mtazamo wa Kikatoliki kuhusu kifo.
Made with FlippingBook Learn more on our blog