The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide
/ 1 1 9
UFALME WA MUNGU
a. Awamu ya kwanza itatokea kwanza wakati wa ufufuo wa wafu waaminio na kubadilishwa kwa Wakristo walio hai wakati wa “unyakuo,” ambao utatokea kabla ya “dhiki kuu” ya Mathayo 24, kipindi cha hofu kuu na hukumu juu ya nchi. (1) Ulimwengu utashuhudia ghadhabu na hukumu ya Mungu wakati wa dhiki kuu. (2) Kanisa litahukumiwa na kupewa thawabu huko mbinguni kwa uaminifu wake.
b. Awamu ya pili itatokea mwishoni mwa hii miaka 7; Kristo atarudi na ufufuo wa wale watakatifu waliokufa wakati wa dhiki kuu.
c. Kiini cha mtazamo huu ni nia ya Kristo kulikoa Kanisa na dhiki kuu, 1 Thes. 5:10.
2. Wanaoamini nadharia ya postribulationism , wanashikilia kwamba kuja kwa Kristo kwa ajili ya watu wake kutatokea mwishoni mwa dhiki kuu.
4
a. Wanakataa aina yoyote ya dhana ya “unyakuo” kuhusiana na kuja kwa Kristo.
b. Nadharia hii inaamini Kanisa litakuwepo wakati wa dhiki kuu.
c. Mtazamo huu pia unatofautisha kati ya ghadhabu ya Mungu na dhiki. (1) Ghadhabu ya Mungu ni hukumu ya Mungu juu ya waovu, Yohana 3:36. (2) Dhiki, kwa upande mwingine, ni kipengele tofauti katika imani ya watakatifu (Yohana 16:33).
Made with FlippingBook Learn more on our blog