The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide
/ 1 3 1
UFALME WA MUNGU
kulingana na uhusiano wake na Mungu katika Kristo, na matokeo ya hukumu yakiwa ya mwisho, yaani yasiyobatilika milele. ³ Hatima ya mwisho wa utimilifu wa Ufalme itasababisha kuondolewa kwa uovu wote, dhiki, na mateso, na hukumu ya shetani. Waliokombolewa watakuwa milki ya pekee ya Mungu, jiji la Mungu litaingia katika milki ya wanadamu, na Kristo ataangusha utawala wote, na mamlaka yote, na nguvu zilizo kinyume na utawala wa Mungu. Shalom ya Mungu itakuja kikamilifu duniani na itadumu milele. ³ Mwishoni, Yesu atawashusha maadui wote chini ya miguu yake pamoja na utawala wote, na mamlaka yote, na nguvu. Hili likikamilika, atakabidhi Ufalme kwa Mungu Baba yake, na katika enzi za enzi, Mungu atakuwa Yote katika yote. Sasa, katika somo hili la mwisho la Kukamilishwa kwa Ufalme wa Mungu, una nafasi ya kuchunguza pamoja na wanafunzi wenzako maswali yako kuhusu Ufalme wa Mungu na kukamilishwa kwake hivi karibuni katika Ujio wa Pili wa Yesu. Muda hautaruhusu kushughulikia kikamilifu na kwa muda mrefu maswali yako, kwa hivyo fikiria kwa bidii. Je, ni masuala gani hasa na mada gani ungependa kuchunguza zaidi kuhusiana na utimilifu wa Ufalme? Huu ni wakati wako wa kuzijadili. Labda baadhi ya maswali hapa chini yanaweza kukusaidia kuunda maswali yako mwenyewe, mahususi na muhimu zaidi. * Je, tunapaswa kufanya nini kuhusiana na mchanganuo wa mambo mengi madogo madogo katika lugha ya ishara na taswira inayohusishwa na unabii wa Biblia kuhusu Ujio wa Pili? Je, kuna njia fulani tunaweza kuzingatia mambo makuu, na kuepuka kupotea katika mambo hayo madogo madogo? * Ni ipi njia bora ya kusisitiza mada za eskatolojia katika huduma yako inayoendelea ya uinjilisti, ufuasi, na mahubiri na ukuaji wa kanisa? * Kwa kuzingatia maoni yote tofauti kuhusu kifo na kufa, hasa sasa kukiwa na mazungumzo mengi ya kiroho katika utamaduni wa kawaida, tunapaswa kusisitiza nini tunapojadili kifo katika viwanja vya umma? * Je, ni muhimu kukazia tazamio la hukumu ya milele kwa wale wasiomjua Mungu? (Makanisa mengi yanayotumia mtazamo wa “kujali hisia za mtafutaji” yangechagua kuepuka aina hii ya mahubiri na mafundisho kwa waliopotea).
Kutendea Kazi Somo na Matokeo yake kwa Wanafunzi
4
Made with FlippingBook Learn more on our blog