The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide

1 6 8 /

UFALME WA MUNGU

Maandiko kuhusu Ufalme katika Agano Jipya (muendelezo)

Luka 9:11 - Na makutano walipojua walimfuata; akawakaribisha, akawa akisema nao habari za ufalme wa Mungu, akawaponya wale wenye haja ya kuponywa. Luka 9:27 - Nami nawaambia kweli, Wapo katika hawa wanaosimama hapa, ambao hawataonja mauti kabisa, hata wauone kwanza ufalme wa Mungu. Luka 9:60 - Akamwambia Waache wafu wawazike wafu wao; bali wewe enenda ukautangaze ufalme wa Mungu. Luka 9:62 - Yesu akamwambia, Mtu aliyetia mkono wake kulima, kisha akaangalia nyuma, hafai kwa ufalme wa Mungu. Luka 10:9 - waponyeni wagonjwa waliomo, waambieni, Ufalme wa Mungu umewakaribia. Luka 10:11 - Hata mavumbi ya mji wenu yaliyogandamana na miguu yetu tunayakung’uta juu yenu. Lakini jueni hili, ya kuwa Ufalme wa Mungu umekaribia. Luka 11:2 - Akawaambia, Msalipo, semeni, Baba [yetu uliye mbinguni], Jina lako litakaswe, Ufalme wako uje, [Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni.] Luka 11:17-18 - Naye akajua mawazo yao, akawaambia, Kila ufalme uliofitinika wenyewe kwa wenyewe hufanyika ukiwa; na nyumba juu ya nyumba huanguka. 18 Basi, ikiwa Shetani naye amefitinika juu ya nafsi yake, ufalme wake utasimamaje? Kwa kuwa ninyi mnasema kwamba mimi natoa pepo kwa Beelzebuli. Luka 11:20 - Lakini, ikiwa mimi natoa pepo kwa kidole cha Mungu, basi ufalme wa Mungu umekwisha kuwajilia. Luka 12:31-32 - Bali utafuteni ufalme wa Mungu, na hayo mtaongezewa. 32 Msiogope, enyi kundi dogo; kwa kuwa Baba yenu ameona vema kuwapa ule ufalme. Luka 13:18 - Kisha alisema, Ufalme wa Mungu umefanana na nini? Nami niufananishe na nini?

Luka 13:20 - Akasema mara ya pili, Niufananishe na nini ufalme wa Mungu?

Made with FlippingBook Learn more on our blog