The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide
1 8 4 /
UFALME WA MUNGU
KIAMBATISHO CHA 18 Mpangilio wa Matukio ya Ufalme wa Mungu Mch. Dkt. Don L. Davis
Mwisho wa Dunia
KALE
Enzi ya Sasa
Enzi Ijayo
Enzi Ijayo
Parousia
Ujio wa Kwanza wa Kristo
Umilele
“Kati ya Nyakati” Tayari Lakini Bado
YESU
Enzi ya Sasa
“Malkuth” ya Yahweh, “basileia tou Theou.” Wayahudi wa Palestina ya karne ya kwanza walimwona Mungu kama Mfalme wa watu wake Israeli na dunia yote. Hata hivyo, kwa sababu ya uasi wa wanadamu na Shetani na malaika zake, utawala wa Mungu duniani bado ni wa wakati ujao . Utakuwa: 1) utaifa – wokovu na utawala wa Israeli juu ya adui zake, 2) ujuzi na utawala wa Mungu ulimwenguni kote, 3) tsidkenu (haki, adili) na shalom (amani), 4) utii kwa Sheria ya Mungu, 5) vita vya mwisho na mataifa ya wasio Wayahudi - Har–Magedoni, 6) kutokea kwa msiba usio wa kawaida utakaotokea mwishoni mwa nyakati, 7) kubadilishwa kwa mbingu na dunia katika fahari ya kabla ya Edeni, 8) utawala wa mwana wa Daudi - mwana wa Adamu, 9) kubatilisha madhara ya laana, 10) ufufuo wa wafu, 11) na hukumu na uharibifu wa maadui wote wa Mungu - dhambi, kifo, uovu, “ulimwengu,” Ibilisi na malaika zake; na 12) uzima wa milele. Tangazo la Yesu: Ufalme wa Mungu sasa umedhihirika katika maisha, nafsi, na huduma ya Masihi Yesu . Kupitia maneno ya Yesu ( kerygma ), matendo yake ya huruma ( diakonia ), miujiza yake, kutoa kwake mapepo, mateso yake, kifo na ufufuo, na kutumwa kwa Roho, Ufalme ulioahidiwa umekuja . Ufalme ni wa sasa na wa wakati ujao ; anatangaza uwepo wa siku zijazo. Baraka za ufalme wa sasa ni pamoja na 1) Kanisa kama ishara na kionjo, 2) ahadi ya Roho Mtakatifu, 3) msamaha wa dhambi, 4) kutangaza Ufalme duniani kote, 5) upatanisho na amani na Mungu, 6) kufungwa kwa Shetani, na huku mamlaka ikikabidhiwa kwa wanafunzi wa Kristo.
Made with FlippingBook Learn more on our blog