The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide

1 9 4 /

UFALME WA MUNGU

Ufalme Wako Uje! Usomaji kuhusu Ufalme wa Mungu (muendelezo)

Zaburi hii moja kwa kweli ina theolojia kubwa ya Ufalme, inayosisitiza enzi kuu ya Mungu, matendo yake makuu, huruma yake na ukaribu wake kwa wale wanaomtafuta, haki na hukumu yake. Ufalme ndio mada kuu ya Maandiko kiasi kwamba Richard Lovelace anaweza kusema, “Ufalme wa Kimasihi si tu mada kuu ya mahubiri ya Yesu; ni dhana kuu inayounganisha ufunuo wa Biblia.” Naye John Bright anaeleza, “Wazo la Ufalme wa Mungu linahusisha, kwa maana halisi, ujumbe kamili wa Biblia. . . . Kufahamu kile kinachomaanishwa na Ufalme wa Mungu ni kuja karibu sana na kiini cha Injili ya wokovu ya Biblia.” Kama E. Stanley Jones alivyoandika zaidi ya miongo minne iliyopita, ujumbe wa Yesu “ulikuwa Ufalme wa Mungu. Ulikuwa ni kiini cha yote aliyofundisha na kufanya. . . . Ufalme wa Mungu ni wazo kuu, mpango mkuu, kusudi kuu, mapenzi makuu ambayo yanakusanya kila kitu ndani yake na kukipa ukombozi, ushikamani, kusudi, lengo.” Ni kweli kwamba kuuona Ufalme wa Mungu kama mada pekee inayounganisha Maandiko kunaweza kupotosha. Binafsi, ninaamini ukweli mkuu ni ufunuo wa asili na tabia ya Mungu (si tu kuwepo kwake, ambako ni dhahiri kupitia uumbaji wake - Warumi 1:20). Hapa kiini ni upendo wa Mungu, haki yake na utakatifu wake – tabia ya Mungu katika utatu wake. Bado utawala/mamlaka ya Mungu ni mada kuu ya Maandiko, kwa kuwa Mungu mwenye upendo, mwenye haki, mtakatifu anatawala kulingana na tabia yake na kwa njia ambayo inaakisi tabia yake kwa wote wanaomtumikia kwa hiari. Kwa hiyo Ufalme kwa hakika ni dhana kuu iliyoenea katika Biblia. Ikiwa haionekani dhahiri sana katika maandiko ya Paulo, ni kwa sababu Paulo mara nyingi anazungumza juu ya Ufalme kama mpango mkuu wa Mungu unaopatikana katika Yesu Kristo (k.m, Waefeso 1:10), na, kwa sababu nzuri sana, hatumii sana lugha ya kifalme. Lakini si sahihi kusema, kama wengine walivyosema, kwamba mada ya ufalme “inatoweka” ndani ya Paulo. . . . Biblia imejaa Ufalme wa Mungu. . . . Tunajifunza zaidi kuhusu Ufalme tunapoona Maandiko yote kuwa historia ya “uchumi” wa Mungu au mpango wa kurejesha uumbaji ulioanguka, na kuleta yote ambayo Mungu ameumba—mwanamke, mwanamume na mazingira yao yote—katika utimilifu wa makusudi yake chini ya utawala na enzi yake kuu. Jioni moja mimi na mwanangu mwenye umri wa miaka saba tulipita kwenye sehemu ndogo ya msitu na tukatoka kwenye uwanja wa wazi. Jua lilikuwa linaelekea magharibi; anga lilikuwa limepambwa kwa bluu na dhahabu tulivu.

Made with FlippingBook Learn more on our blog