The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide

/ 1 9 7

UFALME WA MUNGU

Ufalme Wako Uje! Usomaji kuhusu Ufalme wa Mungu (muendelezo)

wote walijua maana yake. Huu ni mfano mzuri kwetu katika huduma zetu. Yesu alikwenda kwa watu pale walipokuwa (umwilisho!), alikuwa mwaminifu kwa ujumbe wa Biblia, na alizungumza nao kwa maneno ambayo wangeweza kuelewa. (Ona k.m. Luka 1:32-; 19:11; 23:51; Mk. 11:10; 15:43; Mdo. 1:6). Maneno “Ufalme wa Mungu” yaliweka katika muhtasari tumaini na ahadi zote za Agano la Kale. “Yote ambayo Mungu amesema na kufanya katika historia ya Israeli yanakamilika katika Ufalme wa Mungu” (Dale Patrick). 8. L akini Yesu anatoa ufahamu mpya wa dhana ambayo tayari inaeleweka. Anamimina maana yake mwenyewe yenye mamlaka katika Ufalme wa Mungu na kutoa tafsiri mpya ya uhakika ya ahadi na mafundisho ya Agano la Kale. Anathibitisha kwamba “Ufalme wa Mungu” ndio ufunguo wa ufasiri wa Agano la Kale. Anakubaliana na Wayahudi kwamba Ufalme ni Mungu anayekuja katika historia na kutawala kwa kutoa wokovu kwa watu wake na hukumu kwa adui zake. Lakini Yesu anaenda mbali zaidi ya hili katika kutoa tafsiri kuu mpya ya utawala wa Mungu. 9. Y esu anawashtua na kuwashangaza wasikilizaji wake kwa kusema Ufalme wa Mungu ambao wote walikuwa wakiungojea sasa upo (Mk. 1:15). Wakati wa kutimizwa kwa ahadi za Agano la Kale sasa umewadia. Anaenda mbali zaidi ya hilo kwa kufundisha kwamba Ufalme uko ndani yake na katika huduma yake. (Mt. 11:1-15; 12:28; Lk 10:23-; 17:20-). Fundisho hili kwamba Ufalme wa Mungu umefika au uko hapa ni jipya kabisa. Hakuna rabi wa Kiyahudi aliyewahi kufundisha jambo kama hilo (Lk 10:23-). 10. L akini Yesu, kama Wayahudi wengi wa siku zake, pia alifundisha kwamba Ufalme wa Mungu ulikuwa bado wa wakati ujao, yaani, ungekuja baadaye (k.m. Mt 6:10; 8:11-; 25:31-34; Lk 21:31; 22:17-; Mt. 5:3-12; Mk 9:47). 11. S uluhisho la fundisho hili la ajabu ni kutambua kwamba mtazamo mpya wa Yesu kuhusu Ufalme wa Mungu una sura zote mbili: Ufalme upo na unakuja. Yesu alifundisha kuja mara mbili kwa Ufalme. Kwanza, Ufalme ulikuja kwa sehemu katika nafsi yake na huduma yake katika historia. Pili, Yesu alifundisha kwamba kutakuwa na ujio kamili wa wakati ujao wa Ufalme wake atakaporudi mwishoni mwa historia ya wanadamu. 12. S asa tunaweza kuelewa Yesu alimaanisha nini aliposema “siri ya Ufalme” (Mk. 4:10-). Mtazamo huu mpya wa ajabu kuhusu Ufalme wa Mungu ulifundisha kwamba ahadi za Agano la Kale zinaweza kutimizwa bila kukamilishwa.

Made with FlippingBook Learn more on our blog