The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide
/ 3 0 7
UFALME WA MUNGU
Kupingwa kwa Ufalme wa Mungu
MAELEZO YA MKUFUNZI 1
Karibu katika Mwongozo wa Mkufunzi kwa Somo la 1, Kupingwa kwa Utawala wa Mungu . Lengo la jumla la moduli ya Ufalme wa Mungu ni kuwawezesha wanafunzi wako kufahamu nguvu, ajabu, na ukuu wa Ufalme wa Mungu, na maana yake kwa maisha na huduma zao katika makanisa wanamoabudu na kutumika. Somo hili la kwanza limekusudiwa kuwaonyesha wanafunzi jinsi utawala wa Mungu ulivyopingwa katika uasi wa Shetani na kutotii kwa wanandoa wa kwanza wa kibinadamu, na kuzungumzia matokeo ambayo matendo haya yalisababisha juu ya uumbaji wa Mungu. Malengo haya yameelezwa kwa uwazi katika sehemu ya “Malengo ya Somo” na unapaswa kuyasisitiza katika somo lote na wakati wa majadiliano na muda wote uwapo na wanafunzi. Kadiri unavyoweza kuangazia malengo katika kipindi chote cha darasa, ndivyo unavyoongeza uwezekano wa wao kuelewa na kufahamu ukubwa wa malengo haya. Usisite kujadili malengo haya kwa ufupi kabla ya kuingia katika kipindi cha darasa. Vuta usikivu wa wanafunzi kwenye malengo ya somo, kwani, katika maana halisi, hiki ndicho kiini cha lengo lako la kielimu kwa kila kipindi cha darasa katika somo hili. Kila kitu kinachojadiliwa na kufanyika kinapaswa kuwaelekeza kwenye malengo haya. Tafuta njia za kuyaangazia haya kila mara, ili kuyasisitiza na kuyakazia tena na tena kadri unavyoendelea. Ibada hii inawekea mkazo uhakika kamili wa Mungu katika utawala wake akiwa Mungu Mweza-Yote juu ya uumbaji wake. Kwa maana moja somo la leo ni “kejeli”; Mungu hawezi kupingwa kwa njia yoyote ya msingi ambayo inaweza kumfanya aogope, asumbuliwe, au kuzuiwa asitimize kusudi lake. Ibada hii inaweka msisitizo juu ya tabia ya Mungu kuhusu upinzani; anawacheka wale wanaofikiri kwamba wanaweza kupinga mapenzi yake na kutawala kwa mafanikio. Wahakikishie wanafunzi kwamba Mungu ana nguvu kubwa na kuu za kuwashinda adui zake, na uwakumbushe azimio lake la kufanya mapenzi yake duniani kama yanavyofanywa mbinguni.
1 Ukurasa 15 Utangulizi wa Somo
2 Ukurasa 15 Malengo ya Somo
3 Ukurasa 15 Ibada
Wathibitishie wanafunzi wako kwamba Bwana anajua fika kila kitu kuhusu upinzani dhidi ya mapenzi yake, na bado hana chembe hata kidogo ya hisia ya hofu, woga, au kutishwa. Akiwa ndiye Bwana Mwenye Enzi Kuu juu ya Ulimwengu, Bwana
4 Ukurasa 16
Kanuni ya Imani ya Nikea na Maombi
Made with FlippingBook Learn more on our blog