The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide

/ 3 3

UFALME WA MUNGU

MUUNGANIKO

Somo hili limeangazia kweli fulani kuu kuhusu utawala wa Mungu, na upinzani wake kupitia uasi wa Shetani na kutotii kwa Adamu na Hawa. ³ Mungu wa Utatu, YHWH (Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu), ndiye Mwenye Enzi Kuu juu ya ulimwengu, anayeishi kwa kujitegemea mwenyewe, ambaye aliumba ulimwengu ex nihilo kwa utukufu wake. ³ Kama Muumba na Mmiliki wa vitu vyote, enzi kuu ya Mungu imekita mizizi ndani yake, na kudhihirishwa katika kazi zake zote katika uumbaji na matendo yake katika historia. ³ Utawala wa Mungu na haki yake ya kumiliki vilipingwa, mwanzoni na kwa kiasi kikubwa zaidi na shetani katika uasi wake huko mbinguni. ³ Kanuni kuu ya uasi wa kishetani ni kiburi; tamaa yake iliyopotoka ya kupokea heshima na utukufu unaomstahili Mungu pekee. ³ Uasi wa Shetani ulisababisha anguko la malaika wengi waliofuata njia yake, pamoja na jaribu, kutotii, na uasi wa hiari wa Adamu na Hawa katika bustani ya Edeni. Uasi huu mbinguni na duniani unajulikana kama “Anguko.” ³ Matokeo ya kwanza ya Anguko yalikuwa ni kuibuka kwa kosmos , mfumo wa sasa wa ulimwengu usiomcha Mungu ambao unafanya kazi kwa nguvu ya uchoyo, tamaa, na kiburi. ³ Matokeo ya pili ya Anguko yalikuwa kutokea kwa sarx , kupotoshwa na kukengeushwa kwa asili ya mwanadamu, na kusababisha matendo ya dhambi ya kibinafsi, kuingia kwa asili ya dhambi kwa wanadamu (yaani “mwili”), wanadamu wote kuhusishwa na dhambi na hatia kupitia kosa la Adamu, na kifo cha kimwili na kiroho. ³ Matokeo ya tatu ya Anguko na yenye uharibifu zaidi yalikuwa kuachiliwa kwa kakos , ibilisi ambaye sasa anatenda kazi ulimwenguni kama mkufuru dhidi ya Mungu, mdanganyaji wa ulimwengu, na mshitaki wa ndugu. Kupitia Yesu Kristo, tunaweza kumshinda kwa Roho Mtakatifu kupitia Damu ya Mwana-kondoo na neno la ushuhuda wetu, (rej. 1 Yoh. 4:4; Ufu. 12:9-11).

Muhtasari wa Dhana Muhimu

ukurasa 314  19

1

Made with FlippingBook Learn more on our blog