The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide

3 6 /

UFALME WA MUNGU

na kifo. Kadhalika, upinzani huu umeleta matokeo ya kutisha katika nyanja tatu tofauti: kosmos (kuibuka kwa mfumo wa ulimwengu usiomcha Mungu), sarx (dhambi iliyoingizwa na kuenezwa katika asili ya mwanadamu), na kakos (ushawishi unaoendelea na machafuko ya yule Mwovu).

Ikiwa ungependa kufuatilia kwa kina baadhi ya mawazo ya somo hili la Kupingwa kwa Utawala wa Mungu , unaweza kujaribu vitabu hivi: Chapters 1-4 in Beasley-Murray, G. R. Jesus and the Kingdom of God . Grand Rapids: Eerdmans, 1986. “The Ultimate Goal in the Universe” in Billheimer, Paul. Destined for the Throne . Minneapolis: Bethany House, 1975. Chapter 2 in Ladd, George Eldon. The Presence of the Future . Grand Rapids: Eerdmans, 1974. Sasa ni wakati wa kujaribu kukazia theolojia hii ya juu kupitia uhusianishaji katika huduma halisi ya vitendo, ambao utaufikiria na kuuombea katika wiki hii yote ijayo. Roho Mtakatifu anakudokeza nini hasa kuhusiana na utawala wa Mungu, na kupingwa kwake leo? Ni hali gani zinazokuja akilini unapofikiria kuhusu jinsi kweli hii ya utawala wa Mungu inavyopingwa, na pia unapofikiria kuhusu maisha na huduma yako mwenyewe leo? Jipe muda wa kutafakari mbele za Bwana juu ya mambo haya, naye atakupa mafunuo katika eneo hili, na kile unachopaswa kufanya kutokana na kile anachofunua. Weka ahadi ya kumwomba Mungu akupe ufahamu na hekima ya jinsi utawala wake ulivyopingwa mahali unapoishi na kuhudumu. Omba kwamba Mungu Roho Mtakatifu akupe uwezo wa kutoa ushuhuda wa wazi mahali unapoishi na kufanya kazi kuhusu utawala wa ufalme wa Kristo, na fursa ya maisha mapya katika Kristo kama Bwana. Omba kwamba Mungu akupe fursa za kutoa ufafanuzi kwa uwazi na ufanisi kwa wale ambao umeitwa kuhudumia kweli hii kuhusu utawala wa Mungu, kupingwa kwake, na madhara ya upinzani huo katika maisha yao.

Nyenzo na Bibliografia

ukurasa 316  22

1

Kuhusianisha somo na huduma

Ushauri na Maombi

ukurasa 316  23

Made with FlippingBook Learn more on our blog