The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide
6 6 /
UFALME WA MUNGU
Aina ifaayo ya maombi kwa kuzingatia mafundisho ya somo hili ni kuabudu, kusifu, na kushukuru. Kuona azimio la Mungu wa Utatu kuja kutusaidia, kupigana na adui zetu, kupindua athari za Anguko, kumtuma Mwanawe ambaye alimkabili shetani na kifo kwa ajili yetu – upendo huu mkuu unapaswa kuzalisha ndani yetu bubujiko kubwa la sifa na shukrani. Mungu hakutuacha katika hali yetu dhaifu, lakini alitoa kilicho bora kwa ajili yetu. Tunapaswa kutafuta njia za kuonyesha maana ya kutumia ushindi wa Yesu dhidi ya adui zetu na kumwona Mungu akifanya kazi kupitia imani yetu nyenyekevu. Labda kuna watu katika familia yako au kanisani, kazini au katika mtaa wako ambao tunaweza kuwainua kwa Mungu kwa njia ya Yesu.
Ushauri na Maombi
ukurasa 328 15
MAZOEZI
Luka 11:15-20
2
Kukariri Maandiko
Ili kujiandaa kwa ajili ya darasa, tafadhali tembelea www.tumi.org/books ili kupata kazi ya kusoma ya wiki ijayo, au muulize Mkufunzi wako.
Kazi ya Usomaji
Tafadhali soma kwa umakini kazi za usomaji zilizopo hapo juu, na kama wiki iliyopita, ziandikie muhtasari mfupi. Pia, sasa ni wakati wa kuanza kufikiria kuhusu aina ya kazi yako ya huduma kwa vitendo, na pia kuamua ni kifungu gani cha Maandiko utakachochagua kwa ajili ya kazi yako ya ufafanuzi wa Maandiko. Usichelewe kufanya maamuzi juu ya kazi ya huduma kwa vitendo na ile ya ufafanuzi wa Maandiko. Kadiri unavyoamua mapema, ndivyo utakavyopata muda wa kutosha kujiandaa na kutekeleza kazi zako. Kufikia sasa katika moduli hii ya Ufalme wa Mungu tumeangazia Anguko na athari zake, na katika somo hili, tumeona kuhusu azimio la Mungu la kutokomeza athari za Anguko kwa kurudisha utawala wake ulimwenguni kupitia Mwanawe. Inasisimua jinsi gani kujua kwamba Mungu Baba anatupenda sana hivi kwamba alimtuma Shujaa wake bora zaidi, Mwanawe mwenyewe, chini duniani kufanya vita dhidi ya majeshi na nguvu ambazo zilituweka mateka na kufanya maisha yetu kuwa ya huzuni na magumu! Katika somo letu linalofuata tunaangalia jinsi Yesu alivyotoa mamlaka ya ufalme wake kwa watu wake, Kanisa, na jinsi tunavyoitwa sasa kudhihirisha utukufu wake ulimwenguni, na kutenda kama wasaidizi wake, kuthibitisha utawala wake wa ufalme hadi miisho ya dunia.
Kazi Nyinginezo
Kuelekea Somo Linalofuata
Made with FlippingBook Learn more on our blog