The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide
7 6 /
UFALME WA MUNGU
b. Anamtukuza Kristo katikati ya mwili (Yohana 16:14).
c. Anamfunua Kristo kwa waliopotea, Mt. 16:17.
d. Anawaunganisha waamini katika mwili, Efe. 4:3.
e. Anawaita wanaume na wanawake waaminifu kwenye huduma, Mdo. 13:2.
f. Anatoa karama kwa viungo vya mwili kama apendavyo kwa ajili ya kuujenga, 1 Kor. 12:7.
g. Roho Mtakatifu ni Bwana, Roho, akitupatia ishara na maajabu ya nguvu za Ufalme ndani ya kanisa letu la mahali.
3
III. Kanisa pia ndio mahali pa maisha halisi ya ufalme.
Madokezo ya G.E. Ladd kuhusu Ufalme: • Kanisa si Ufalme, bali ni udhihirisho wa Ufalme. • Ufalme huunda Kanisa. • Kanisa linashuhudia habari za Ufalme ulimwenguni. • Kanisa ni chombo cha Ufalme. • Kanisa ni mlinzi [wakala] wa Ufalme.
A. Ufalme wa Mungu unadhihirika katika maisha na ushuhuda wa Kanisa.
1. Utukufu wa Mungu wa Shekina unadhihirika sasa katika Kanisa kupitia nafsi ya Roho Mtakatifu, Efe. 2:21-22.
Made with FlippingBook Learn more on our blog