The Kingdom of God, Swahili Student Workbook
1 0 8 /
UFALME WA MUNGU
a. Mara tu baada ya mtu kufa, hali yake ya milele inaamuliwa.
b. Wale wanaokufa katika hali ya uovu huenda moja kwa moja kuzimu, mahali pa mateso, wakati wale walio katika hali ya neema na kutakaswa wakati wa kifo huenda moja kwa moja mbinguni.
c. Wale walio katika hali ya neema, ambao bado hawajakamilika kiroho huenda toharani, mahali pa adhabu ya muda, kwa wale ambao hawajajiweka huru kabisa na dhambi zao mbaya au makosa yao.
d. Thomas Aquinas, msomi wa kwanza Mkatoliki wa karne ya 12, alieleza jinsi wale walio katika toharani wanavyoweza kusaidiwa. (1) Kupitia Misa. (2) Kupitia maombi ya watakatifu. (3) Kupitia matendo mema ya waumini walio hai.
4
2. Ushahidi wa Kibiblia: “Bali yeye atakayenena neno juu ya Roho Mtakatifu hatasamehewa katika ulimwengu wa sasa, wala katika ule ujao,” Mt. 12:32.
a. Andiko hili linasomwa ili kujenga hoja ya kwamba kuna madaraja (viwango) kati ya dhambi.
b. Hiyo ingemaanisha kwamba dhambi zingine (zaidi ya kumkufuru Roho Mtakatifu) zitasamehewa katika ulimwengu ujao.
c. Toharani ni fundisho ambalo linaonekana kuwa matokeo ya kimantiki ya tafsiri hii ya Maandiko.
Made with FlippingBook - Online catalogs