The Kingdom of God, Swahili Student Workbook

/ 1 0 9

UFALME WA MUNGU

3. Je, mtazamo huu unashawishi? Hapana, kwa sababu kadhaa:

a. Ni mtazamo unaodokeza aina fulani ya matendo ya haki, jambo ambalo ni kinyume na mafundisho mengi ya wazi ya Agano Jipya, hasa Wagalatia 3:1-14 na Waefeso 2:8-9.

b. Kiini cha mafundisho ya Agano Jipya ni kwamba tunaokolewa kwa neema kwa njia ya imani, si kwa matendo yetu.

c. Theolojia ya toharani kimsingi inazungumza juu ya wafu kuwekwa katika aina fulani ya uangalizi wa kiroho, dhana ambayo inadokeza uwezekano wa jitihada fulani za kibinadamu za kusaidia katika kumwezesha mtu kupata haki mbele za Mungu. Hii haiwezi kukubalika.

D. Hali ya wafu kama tumaini la mwamini: kusafirishwa katika uwepo wa Bwana.

4

1. Maelezo ya jumla kuhusu hali ya wafu.

a. Hali ya wafu wasio haki haiko wazi kabisa katika Maandiko, ingawa mafundisho ya Yesu juu ya tajiri katika Luka 16 yangechukuliwa kama yenye kutofautiana na dhana ya “usingizi wa roho,” na badala yake kinachoonekana ni aina ya huzuni na mateso kuzimuni.

b. Hata hivyo, Biblia hutoa dalili kwamba wafu waadilifu hawapotezi fahamu au kuingia katika hali ya utusitusi (hali fulani ya giza) kuzimuni.

2. Je, ni upi mtazamo kwa habari ya waamini wanaotumaini uwepo wa Bwana?

Made with FlippingBook - Online catalogs