The Kingdom of God, Swahili Student Workbook
1 1 2 /
UFALME WA MUNGU
Kukamilishwa kwa Utawala wa Mungu Sehemu ya 2
Mch. Dkt. Don. L. Davis
Mambo ya jumla yanayohusiana na kukamilishwa kwa Ufalme wa Mungu ni Ujio wa Pili wa Yesu Kristo, ufufuo wa wafu na hukumu ya mwisho, na Mungu kuwa Yote-katika-yote. Malengo yetu ya sehemu hii ya pili ya Kukamilishwa kwa Utawala wa Mungu ni kukuwezesha: • Kubainisha vipengele muhimu vinavyohusiana na Ujio wa Pili wa Yesu Kristo ili kukamilisha Ufalme wa Mungu duniani. • Kueleza waziwazi mafundisho ya Maandiko yanayohusiana na ufufuo wa wafu na hukumu ya mwisho. • Kufahamu hali ya mwisho ya Ufalme uliokamilishwa, wakati Mungu Mwenyezi atakapokuwa Yote katika yote kwetu.
Muhtasari wa Sehemu ya 2
4
I. Ufalme Utakamilika Katika Ujio wa Pili wa Yesu Kristo.
Muhtasari wa Sehemu ya 2 ya Video
A. Ujio wa Yesu Kristo ( parousia ) hakika utatokea, na utakuwa wa uhakika.
1. Parousia , ambayo inaweza kutafsiriwa kama “kuwapo” au “kuja” mara nyingi huhusishwa na kurudi kwa Yesu, ambako alitaja mara nyingi katika mafundisho yake, kama vile katika Mathayo 24:30 na 26:64.
2. Petro anarejelea uhakika wa kuja kwa Yesu, Mdo. 3:19-21.
3. Paulo hana shaka na Roho wa Bwana kuthibitisha uhakika wa kuja kwa Kristo, 1 Thes. 4:15-16.
Made with FlippingBook - Online catalogs