The Kingdom of God, Swahili Student Workbook

/ 1 1 3

UFALME WA MUNGU

4. Kwa Yesu na Mitume, Ujio wa Pili wa Yesu ulikuwa wa kweli, wa uhakika, na usioweza kutiliwa shaka kabisa.

B. Ujio wa Pili wa Yesu Kristo pia uko karibu (unaweza kutokea wakati wowote).

1. Parousia iko karibu na haijulikani siku.

a. Yesu alisema kwamba si yeye, wala malaika, wala mtu ye yote ajuaye wakati wa kuja kwake, ila Baba yake, Mk 13:32-33 na Mt. 24:36-44.

b. Baba ameweka wakati na majira katika mamlaka yake mwenyewe, Mdo 1:7.

c. Kwa kuwa ujio huo haukujulikana, Mitume walitoa mahusia mengi ya kuwa macho, kuwa na kiasi, na kuwa tayari kwa ajili ya kurudi kwake karibuni, lakini kusikojulikana siku wala saa, 1 Thes. 5:6-9.

4

C. Ujio wa Pili wa Yesu Kristo utakuwa wa utukufu na fahari. Hali yake itakuwaje?

1. Ujio wake utakuwa wa kibinafsi .

a. Ahadi ya Yesu kwa wanafunzi, Yohana 14:3

b. Ushuhuda wa Paulo wa kuja kwa Bwana, 1 Thes. 4:16

Made with FlippingBook - Online catalogs