The Kingdom of God, Swahili Student Workbook

1 1 6 /

UFALME WA MUNGU

b. Hata hivyo, maandiko kama 1 Wathesalonike 4:16, 2 Wathesalonike 2:8, na Mathayo 24:27 yanahusisha neno parousia na tukio la wazi lenye nguvu, moja, na la pamoja.

c. Watakatifu wanangojea tumaini moja lenye baraka (si matumaini kadhaa) na kufunuliwa (si awamu za kufunuliwa) kwa utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu (Tito 2:13).

II. Maoni mbalimbali ya Milenia na Dhiki Kuu yanayohusishwa na Ujio wa Pili wa Yesu Kristo

A. Swali la milenia linalobishaniwa ni kama kutakuwa na milenia au la (utawala wa miaka 1,000 wa Yesu Kristo duniani), na kama ni hivyo, itatokea kabla au baada ya kuja kwake.

1. Nadharia ya Ujio wa Baada ya Milenia ( Postmillennialism) inatokana na wazo kwamba mahubiri ya Yesu yatafanikiwa sana kiasi kwamba ulimwengu mzima utaongoka, na utawala wa Kristo utakuwa ni utawala kamili na wa ulimwengu wote.

4

a. Nadharia hii imejengwa kwa kutumia mistari kama Isaya 45:22-25

b. Ilikuwa maarufu zaidi nyakati ambazo Kanisa lilifanikiwa katika kuleta mabadiliko ya kisiasa au kijamii.

c. Imepoteza uungwaji mkono kufuatia vita vya ulimwengu vya karne ya 20 na uharibifu mkubwa na ukosefu wa haki wa nyakati za sasa.

2. Nadharia ya Premilenia au Ujio wa Kabla ya Milenia ( Premillennialism ) inaamini katika utawala halisi wa Kristo duniani kwa takriban miaka elfu moja baada ya kurudi kwake.

Made with FlippingBook - Online catalogs