The Kingdom of God, Swahili Student Workbook
/ 1 1 7
UFALME WA MUNGU
a. Inaitwa “ chialism ” (Kiyunani cha 1,000); mtazamo huu ulikuwa mtazamo mkuu wa karne tatu za kwanza za Kanisa, na ulikua maarufu katika duru za kihafidhina katika karne ya 19.
b. Andiko kuu: Ufunuo 20:4-6. (1) Utawala halisi wa miaka elfu moja. (2) Ufufuo katika awamu mbili (moja kabla ya milenia kwa ajili ya wenye haki, na wa pili baada ya milenia kwa ajili ya waovu).
c. Kipindi cha miaka 1,000 kitatokea baada ya dhiki kuu, ambapo Kristo atakuja na kuanzisha kipindi cha amani na haki.
3. Nadharia ya Amilenia ( amillennialism ) inadai kwamba hakutakuwa na milenia, hakuna utawala wa kidunia wa Kristo.
a. Hukumu kuu na ya mwisho inakuja baada ya Ujio wake wa Pili.
4
b. Hali za milele za wanaoamini na wasioamini zitaanzia wakati huo.
c. Katika nadharia hii kitabu cha Ufunuo kinatafsiriwa kwa kiasi kikubwa kama ishara na mifano tu.
d. Nadharia hii inadai kwamba mtazamo huu ni rahisi kuliko maoni ya baada ya au kabla ya milenia, na inachukulia kutajwa kwa milenia, kama inavyochukulia vitu vingine vingi katika Ufunuo, kwa kiasi kikubwa katika maana ishara.
4. Tamko kuhusu nadharia hii ya Amilenia
Made with FlippingBook - Online catalogs