The Kingdom of God, Swahili Student Workbook

1 1 8 /

UFALME WA MUNGU

a. Kesi ya mtazamo wa amilenia (1) Mtazamo wa ujio wa baada ya milenia unaonekana kwenda kinyume na fundisho la wazi la Yesu kwamba uasi mkuu na ukengeufu ungeambatana na Ujio wake wa Pili. (2) Mtazamo wa amilenia unashindwa, katika sehemu fulani, kuchukulia maneno ya kinabii kwa uzito, ukiyaweka Maandiko yote ya kinabii katika maana za mifano. (3) Kwa sifa yake, nadharia ya ujio wa ya kabla ya milenia inaelekea kupatanisha idadi kubwa ya Maandiko, na inaonekana hakuna vifungu vya Biblia ambavyo vinakinzana moja kwa moja na mtazamo huu. (4) Labda jambo lenye nguvu zaidi ni madokezo ya Biblia kuhusu ufufuo wa kikundi au hatua mahususi, Luka 14:14; 20:35; 1 Kor. 15:23; 1 Thes. 4:16; Dan. 12:2, na Yohana 5:29. b. Kuelewa jambo kuu: Ufalme utakamilishwa na Yesu katika wakati wa Mungu mwenyewe. (1) Wanafunzi wa Maandiko hutofautiana katika maoni yao hapa. (2) Muhimu zaidi kuliko mtazamo wowote ule ni uhakika wa kurudi kwa Bwana wetu, na uhakika kwamba atakamilisha Ufalme, katika wakati wa Mungu.

4

B. Swali la dhiki linalobishaniwa ni ikiwa Yesu Kristo atawaondoa watu wake kutoka ulimwenguni kabla ya dhiki kuu (inayoitwa pretribulationism ), au ikiwa Yesu atarudi baada ya dhiki kuu ( postribulationism ), au ikiwa atarudi katikati ya kipindi cha dhiki kuu ( midtribulationism ).

1. Wanaoamini katika nadharia ya pretribulationism , yaani kurudi kwa Kristo Kabla ya Dhiki Kuu wanashikilia kwamba kutakuwa na awamu mbili za kuja kwa Kristo.

Made with FlippingBook - Online catalogs