The Kingdom of God, Swahili Student Workbook

1 2 0 /

UFALME WA MUNGU

d. Nadharia ya Kurudi kwa Kristo baada ya dhiki kuu ( posttribulation ) inaamini kwamba Mungu atawategemeza watu wake katikati ya dhiki kuu.

3. Nadharia ya midtribulation inatafuta kutatua mzozo kati ya nadharia ya kabla na ile ya baada ya dhiki. Inadai kwamba Kanisa litapatia nusu ya kwanza ya kipindi cha dhiki kuu, ambayo kwa mujibu wa nadharia hii kitakuwa kipindi cha mateso yasiyo makali sana, na kisha litaondolewa kabla ya kuanza kwa nusu ya pili, wakati Mungu atakapomimina ghadhabu yake juu ya dunia.

a. Kwa hiyo Kanisa, kwa mtazamo huu, litapitia dhiki lakini litaepushwa na ghadhabu ya Mungu.

b. Nadharia hii inawakilisha mtazamo wa kati kati ya mtazamo wa “kabla” na wa “baada” ya dhiki.

4

4. Jambo kuu zaidi: Uwezo wa Mungu wa kutegemeza walio wake wakati wa shida.

a. Ladha ya jumla ya mafundisho ya Biblia kuhusiana na majaribu na mitihani inaonekana kuendana na mtazamo wa “baada” ya dhiki.

b. Maandiko yamejaa maangalizo ya kutoepukika kwa waamini kupitia majaribu mbalimbali, Yakobo 1:3 na 1 Pet. 4:12.

c. Ni lazima tuwe tayari kuvumilia chochote ambacho Mungu anaweza kuruhusu kwenye maisha yetu.

d. Tunaweza kuwa na uhakika kwamba chochote ambacho Mungu anasema au kuruhusu, neema yake itatupa nguvu za kuvumilia na kusimama.

Made with FlippingBook - Online catalogs