The Kingdom of God, Swahili Student Workbook

1 2 4 /

UFALME WA MUNGU

3. Kiwango cha Yesu: kipimo cha maarifa ambacho mtu alikuwa nacho cha mapenzi ya Mungu yaliyo wazi, Mt. 11:21-24.

C. Hukumu ya mwisho inajumuisha wanadamu wote: kila mwanadamu atahukumiwa, Mt. 25:32; 2 Kor. 5:10; Ebr. 9:27.

1. Kila mtu atatoa hesabu yake mwenyewe kwa Mungu kama Paulo anavyoonya katika Warumi 14:10-12.

2. Wakristo na wasio Wakristo watahukumiwa, hata hivyo, hukumu itatendeka kwa misingi tofauti sana.

D. Hukumu ya mwisho itategemea uhusiano wa mtu na Mungu katika Yesu Kristo.

1. Hukumu hii inategemea kile mtu anachoamini kuhusu utu na kazi ya Yesu Kristo (Yohana 3:36).

4

2. Aliye naye Mwana, na yeye asiye naye Mwana, 1 Yoh 5:11-13

3. Kupimwa kwa kazi ya mwamini wakati ujao, 1 Kor. 3:12-15

E. Hukumu ya mwisho itakuwa ya mwisho .

1. Wale wasiomjua Mungu watakuwa chini ya hukumu ya Mungu isiyoisha.

2. Hukumu haitaweza kutenguliwa, kwa mujibu wa Luka 16:19-31.

Made with FlippingBook - Online catalogs