The Kingdom of God, Swahili Student Workbook

/ 1 2 5

UFALME WA MUNGU

3. Angalia ukweli wa kutisha wa hitimisho linalohusishwa na hukumu hii katika Mathayo 25:41.

4. Fundisho kuhusu “kuangamiza.”

a. Mtazamo huu unadokeza kwamba ingawa si kila mtu ataokolewa (dhana inayoitwa “wokovu wa ulimwengu wote”), wasio haki wataharibiwa na kuangamizwa; wataondoshwa wasiwepo milele.

b. Nadharia hii inaamini kwamba waovu wataondoshwa wasiwepo kabisa, huku waadilifu wakiendelea kufurahia baraka za Mungu zisizo na mwisho.

c. Ingawa mtazamo huu unapata umaarufu fulani sasa, ni lazima tuzingatie lugha inayohusishwa na hukumu iliyotolewa katika Maandiko, tukizungumza juu ya hali yake uendelevu. (1) Hukumu inahusishwa na “moto usiozimika,” Mk 9:48.

4

(2) Kuchomwa milele, Mt. 25:41 (3) Dharau ya milele, Dan. 12:2 (4) Uharibifu wa milele, 2 The. 1:9 (5) Mateso ya milele, Ufu. 14:11 (6) Adhabu ya milele, Mt. 25:46.

Made with FlippingBook - Online catalogs