The Kingdom of God, Swahili Student Workbook
1 2 8 /
UFALME WA MUNGU
d. Mungu Mwenyezi, Mungu wa Utatu, atakuwa Yote-katika-yote.
Maranatha! Amina, njoo, Bwana Yesu!
Hitimisho
» Ufalme utakamilika katika Ujio wa Pili wa Yesu Kristo.
» Katika utimilifu huo, Mungu Mwenyezi katika Yesu atashinda kifo, na kusababisha ufufuo wa wafu na hukumu ya mwisho juu ya wanadamu. » Hatimaye, mwishoni, hata Ufalme wenyewe utafanywa kuwa chini ya Mungu Mwenyewe, ili kwamba Mungu apate kuwa Yote katika yote.
Maswali yafuatayo yaliundwa ili kukusaidia kufanya marudio ya maudhui ya sehemu ya pili ya video inayohusiana na Ujio wa Pili wa Yesu, pamoja na masuala ya kifo, hali ya wafu, ufufuo, hukumu ya mwisho, na utimilifu wa mwisho wa Ufalme pamoja na Mungu kama Yote-katika-yote. Jibu maswali, ukizingatia “mawazo makubwa” na kanuni zinazohusiana na utimilifu, hasa juu ya jukumu la Yesu katika kukamilisha Ufalme katika Ujio wake wa Pili. Jibu kwa uwazi na kwa ufupi, na inapowezekana, tumia Maandiko! 1. Nini maana ya neno la Kiyunani parousia ? Je! Neno hili linatusaidiaje kuelewa Ujio wa Pili wa Kristo? 2. Ni kwa njia gani tunajua kwamba Ujio wa Pili wa Yesu ni wa kweli, wa uhakika, na usioweza kutiliwa shaka kabisa? Je, tunamaanisha nini tunaposema kwamba ujio wake “uko karibu lakini haujulikani siku?” 3. Eleza maana mbalimbali zinazohusishwa na sifa tukufu za kurudi kwa Yesu hivi karibuni (k.m. ni kwa kibinafsi, katika mwili, wa wazi/ unaoonekana, uliojaa fahari na utukufu, na usiotarajiwa). Kwa nini kila moja ya haya ni muhimu ili kuelewa asili ya kweli ya parousia ? 4. Eleza tofauti kati ya maoni mbalimbali ya milenia (baada ya milenia, kabla ya milenia, na katikati ya milenia) ya Ujio wa Pili. Ni maoni gani yanaonekana kuakisi vizuri zaidi kile ambacho Maandiko yanafundisha juu ya milenia?
Sehemu ya 2
Maswali kwa Wanafunzi na Majibu
4
Made with FlippingBook - Online catalogs