The Kingdom of God, Swahili Student Workbook
/ 1 2 9
UFALME WA MUNGU
5. Eleza tofauti za mitazamo mbalimbali juu ya dhiki kuu (maoni ya kabla ya dhiki, baada ya dhiki, na katikati ya dhiki). Ni maoni gani yanaonekana kuakisi vizuri zaidi kile Maandiko yanafundisha juu ya dhiki kuu? 6. Jadili pamoja baadhi ya vipengele muhimu vinavyohusiana na ufufuo. Kuna tofauti gani kuu kati ya ufufuo wa wenye haki na ule wa wasio haki? 7. Ni zipi baadhi ya sifa muhimu zaidi zinazosemwa katika Maandiko kuhusu hukumu ya mwisho? Yesu ana jukumu gani katika hukumu hiyo, na mwisho wa wale wote wanao husika kupokea hukumu hiyo utakuwa nini? 8. Eleza sifa za ulimwengu uliorejeshwa upya na mbingu mpya na nchi mpya wakati wa kukamilishwa kwa Ufalme. Uumbaji utabadilikaje? Vipi kuhusu nafasi ya watakatifu katika mbingu mpya na nchi mpya? 9. Mwishowe, Yesu atafanya nini na Ufalme wakati maadui wote watakapowekwa chini ya miguu yake? Je, jukumu la Mungu litakuwa nini katika enzi za enzi zijazo? Somo hili linaangazia juu ya kukamilishwa kwa Ufalme wa Mungu katika Ujio wa Pili wa Yesu Kristo, ambaye hivi karibuni atafunuliwa na atasimamisha utawala wake duniani. Parousia ni neno linalohusishwa na kurudi kwa Yesu, tendo ambalo litakuwa la kibinafsi, katika mwili, linaloonekana, la utukufu, na la upesi. Utimilifu wa Ufalme huo unafungamana kabisa na yale ambayo Biblia inafundisha kuhusu kifo, ufufuo, na hukumu ya mwisho. Maadui wote watakapowekwa chini ya miguu ya Yesu, atakabidhi Ufalme kwa Mungu Baba yake ili Mungu awe Yote-katika yote. ³ Eskatolojia ni neno la kitheolojia linalohusishwa na elimu ya mambo ya mwisho, na parousia ni neno linalohusishwa na Ujio wa Pili wa Yesu Kristo. ³ Tunapaswa kuwa na bidii na uangalifu katika kujifunza fundisho la mambo ya mwisho (kukamilishwa kwa Ufalme) kwa sababu ya uwezo wake sio tu wa kuathiri hali yetu ya kukesha, kiasi, na utakatifu wetu mbele za Mungu, bali pia uwezo wetu wa kuhudumu na kuwafariji wale wanaohuzunika kwa sababu ya kupoteza wapendwa wetu. ³ Eskatolojia ya kibinafsi inahusu matukio yanahusu hatima inayowangoja watu binafsi siku zijazo, wakati eskatolojia ya ulimwengu inahusu yale yatakayowapata jamii nzima ya binadamu na viumbe vyote.
MUUNGANIKO
Muhtasari wa Dhana Muhimu
4
Made with FlippingBook - Online catalogs