The Kingdom of God, Swahili Student Workbook

1 3 0 /

UFALME WA MUNGU

³ Kuhusiana na fundisho la Biblia kuhusu kifo, tunajua kwamba kifo ni halisi na hakiepukiki kwa watu wote, kwamba asili ya kifo ni ya kimwili (mwisho wa maisha na kutenganishwa kwa mwili na nafsi), na ya kiroho (kutengwa kwa mtu na Mungu). Mauti yote, ya kimwili au ya kiroho, ni matokeo ya dhambi zilizotendwa na hukumu ya Mungu. ³ Ingawa kifo ni janga na adhabu kwa asiyeamini, kifo si laana tena kwa Mkristo, kwa kuwa Yesu amekuwa laana kwa ajili yetu. Ingawa kifo cha kimwili kinaweza kuwa hakika kwa waamini, kufa kama Mkristo ni kusafirishwa mara moja hadi kwenye uwepo wa Bwana. Kwa wasioamini, si dhana ya “usingizi wa nafsi” wala ile ya “toharani” inayonekana kuelezea ukweli wa kibiblia wa hali zao baada ya kufa, bali ni aina fulani ya mateso kuzimuni, huku wakingojea hukumu. ³ Ufalme wa Mungu utakamilika katika Ujio wa Pili wa Yesu Kristo, ambao utakuwa wa uhakika, wa ghafla, usiojulikana kwa wote isipokuwa Baba, wa kibinafsi, wa kimwili, unaoonekana, uliojaa fahari na utukufu, na usiotarajiwa. Litakuwa kuwa tukio moja, ingawa tukio hilo moja la kuja kwake linaweza kuhusisha awamu na hatua tofauti. ³ Swali la milenia linatafuta kujibu ikiwa kutakuwa na milenia (kipindi cha miaka 1,000 ya utawala wa Yesu Kristo duniani), na ikiwa ndivyo, itatokea lini (kabla au baada ya kuja kwake). Nadharia ya ujio wa Kristo baada ya Milenia inaamini mahubiri ya Yesu yatafanikiwa sana hata ulimwengu mzima utaongoka. Nadharia ya ujio wa Kristo kabla ya Milenia inaamini kwamba Yesu atarudi kabla ya kipindi cha miaka 1,000, na kutawala kiuhalisi duniani. Nadharia Amilenia inadai kwamba hakutakuwa na milenia au utawala wa kidunia wa Kristo. Ingawa maoni yote yana ugumu fulani, mtazamo wa ujio wa Kristo kabla ya Milenia unaonekana kuoanisha mafundisho ya kimaandiko vyema zaidi. ³ Swali la dhiki kuu linauliza kama Yesu atawaondoa watu wake duniani kabla ya dhiki kuu ( pretribulationism ), wakati wa dhiki kuu ( midtribulationism ), au baada ya dhiki kuu (p osttribulationism ). Hata iwe ni wakati gani, Mungu ameahidi kuwapa watu wake nguvu zote zinazohitajiwa ili kuvumilia majaribu kwa ajili ya utukufu wake mkuu zaidi. ³ Biblia inafundisha bila shaka ufufuo wa wafu. Ufufuo huu utakuwa wa uhakika, utahusisha kazi ya Mungu wa Utatu, na utakuwa ufufuo halisi na wa kimwili. Pia kutakuwa na ufufuo wa wenye haki na wa wasio haki. Kwa njia hiyohiyo, hukumu ya mwisho itakuwa ya wakati ujao, Yesu Kristo akiwa Hakimu Mkuu. Hukumu yake itahusisha kila mwanadamu,

4

Made with FlippingBook - Online catalogs