The Kingdom of God, Swahili Student Workbook

/ 1 9 1

UFALME WA MUNGU

KIAMBATISHO CHA 21 Ufalme Wako Uje! Usomaji kuhusu Ufalme wa Mungu Imehaririwa na Terry G. Cornett na Don L. Davis

Hadithi ya Falme Mbili

Imetokana na “The Agony and Ecstasy” ndani ya Why We Haven’t Changed the World, na Peter E. Gillquist. Old Tappan, New Jersey: Fleming H. Revell Company, 1982. uk. 47-48.

Sikia mfano wa ufalme, mfalme mnyang’anyi wa ulimwengu huu. Kupitia mkakati stadi wa udanganyifu uliojaa werevu wa ajabu, amefaulu kuleta mamilioni ya raia chini ya utawala wake wenye nguvu. Ni kweli kwamba amewavuta kutoka katika milki ya Mfalme mwingine, lakini anawaona kuwa ni mali yake. Hata hivyo, wamekuwa chini ya utawala wake kwa muda mrefu sasa, na Adui bado hajawachukua tena. Ndiyo, kwa mawazo ya mfalme huyu, watu hawa kisheria ni watu wake na nchi hii ni nchi yake. Hata hivyo, anasema, “umiliki ni tisa ya kumi ya sheria.” Ghafla, bila onyo kubwa, Serikali pinzani inachukua hatua. Mwana Mfalme wa Adui anatumwa katika himaya ya mfalme mwenyewe (naam, ndio, aliiba, lakini. . . .) ili kuwarudisha wale ambao wangejitiisha tena kwa utawala wake. Mpango wa Mfalme ni kuwatoa watu hawa chini ya mamlaka, falsafa na mtindo wa maisha wa mfalme. Jambo la kuchukiza zaidi kuliko yote, Mfalme anaweka Serikali yake kwenye himaya ya mkuu mwenyewe. Na badala ya kuwaondoa mara moja raia wake waliorejeshwa kutoka nchi hiyo, anawaweka huko mpaka ugonjwa uitwao kifo (matokeo ya utawala wa mfalme ambayo hatimaye yanamkabili kila mtu) ulete mabadiliko katika hali ya uwepo wao. Ili kufanya jambo hilo liwe baya zaidi, Mwana hata anawaahidi watu kwamba atawaokoa na kifo, na kwamba yeye mwenyewe atafanyika limbuko kwa kufa na kufufuka tena. Akiwa amekoseshwa utulivu kwa ujumbe huo, lakini hajashindwa (ndivyo anavyodhani), mfalme anaanzisha mashambulizi ya pande zote. Kilicho dhahiri ni kwamba hawezi kabisa kukabiliana na Mfalme yule mwingine uso kwa Uso. Kwa hiyo anazindua mpango mpya wa udanganyifu, akiwadanganya tu wananchi wake kuhusu Serikali ile nyingine. Mbinu hiyo haifanyi kazi nyakati zote, maana Mwana Mfalme anaendelea kurejesha watu chini ya utawala wake. Kwa kuwa wao ni viumbe dhaifu, hata hivyo, mfalme haoni sababu ya kukata tamaa ya kurudi kwao hatimaye. Kwa hiyo, hata baada ya wao kuwa raia wa ufalme huo mwingine, anaendeleza shinikizo. Udanganyifu ndio silaha kubwa ya mfalme. Anaitumia katika maeneo ya kimkakati zaidi. Kwa kuwa watu waliojitoa zaidi ndio hatari zaidi, anawashambulia wakereketwa miongoni mwa raia wake wa zamani kwa kueneza uvumi juu yao na kuwatisha kwa vidokezo vya uwezo wake. Kwa kiasi kikubwa mafanikio yake ni

Made with FlippingBook - Online catalogs