The Kingdom of God, Swahili Student Workbook

1 9 2 /

UFALME WA MUNGU

Ufalme Wako Uje! Usomaji kuhusu Ufalme wa Mungu (muendelezo)

madogo, hata hivyo, kwa sababu watu hawa wanaonyesha uhusiano wa karibu usio wa kawaida kwa Mfalme Adui. Bado, mfalme huyo anatiwa moyo na chanzo kimoja kidogo, ingawa ni chanzo muhimu, cha msaada ambacho hakuwa ametegemea. Kuna baadhi ya watumishi wa Mwana wa Mfalme wanaoelezea vibaya ahadi zake, japokuwa wengi wao ni waaminifu na wenye nia njema. Watumishi hawa wamedhamiria sana kuwarudisha watu kutoka katika himaya ya mfalme mwovu, kiasi kwamba katika jumbe zao wanaacha mambo muhimu sana kuhusu uwajibikaji kama raia katika himaya hiyo. Mara chache sana, kama imewahi kutokea, wanataja vita, au mbinu za uasi za mfalme mwovu, au matokeo ya mabaki ya magonjwa ya kutisha yaliyopatikana chini ya utawala wake. Kwa kweli, wao huonyesha Serikali ya Mwana kama aina fulani ya ustawi wa kiroho, ambapo kuna manufaa ya bure kwa wote, kwa kazi au wajibu mdogo sana. Mtu anapata picha ya aina fulani ya paradiso rahisi, ambamo Mfalme anaendesha mpango kabambe wa zawadi. Kwa furaha, mkuu mwovu anatumia udhaifu huu wa kutoelezea vizuri mambo. Anachofanya ni kuwaacha wahubiri mapungufu haya na kisha ajinufaishe kwa kutumia mikanganyiko ambayo watu wanakabiliana nayo katika maisha yao ya kila siku. Kwa kweli, chanzo chake bora zaidi cha wanaorudi kwake huenda kikawa ni wasikilizaji waliokatishwa tamaa wanaowasikiliza watumishi hao wenye shauku. Yesu alijawa na mambo ya kushangaza siku zote, hata akiwa na wanafunzi wake. Labda jambo la kushangaza zaidi lilikuwa habari zake kuhusu Ufalme wa Mungu. Yesu alikuja akitangaza Ufalme, na hivyo kusababisha ghasia. Kupitia kipindi kifupi cha huduma yake ya hadharani aliendelea kuwaonyesha wanafunzi wake jinsi Ufalme ulivyokuwa hasa. Walielewa kwa sehemu tu. Baadaye, alipofufuka katika wafu, Yesu alitumia majuma sita akiwafundisha wanafunzi wake zaidi kuhusu Ufalme (Mdo. 1:3). Aliwaeleza kwamba mateso yake, kifo na ufufuo wake mwenyewe vyote vilikuwa sehemu ya mpango wa Ufalme uliotabiriwa na manabii wa Agano la Kale (Luka 24:44-47). Sasa, baada ya ufufuo, wanafunzi wake wanauliza, “Kwa hiyo, hatimaye utausimamisha Ufalme wako?” (ufafanuzi wa Matendo 1:6). Yesu anajibuje? Anasema, kwa maneno mengine, “Wakati wa kuchanua kabisa kwa utaratibu mpya Ufalme kama Ufunguo wa Maandiko Yote

Inatokana na kitabu cha “Introduction and Chapter One” in A Kingdom Manifesto, cha Howard A. Snyder. Downers Grove: InterVarsity Press, 1985. uk. 11-25

Made with FlippingBook - Online catalogs