The Kingdom of God, Swahili Student Workbook

/ 1 9 3

UFALME WA MUNGU

Ufalme Wako Uje! Usomaji kuhusu Ufalme wa Mungu (muendelezo)

ungali fumbo kwenu; huo uko mikononi mwa Mungu. Lakini. . . . Roho Mtakatifu atakupeni nguvu za kuishi maisha ya Ufalme sasa. Kwa hiyo mtakuwa mashahidi wa Ufalme na nguvu zake kuanzia hapa hata miisho ya dunia” (Matendo 1:7-8). Na ndivyo ilivyokuwa, na ndivyo ambavyo imekuwa. Leo hatimaye tunakaribia kuona unabii wa Yesu ukitimia, kwamba “habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote” (Mt. 24:14). Na kwa hiyo, kuliko wakati mwingine wowote, huu ni wakati wa kuzungumza kuhusu Ufalme wa Mungu sasa! Hili si jaribio la kubashiri makusudi ya Mungu au kufumbua fumbo kuu la Ufalme kabla ya wakati. Ufalme bado na daima unabaki mikononi mwa Mungu. Kwa hiyo kitabu hiki hakihusu “nyakati au tarehe” (Mdo. 1:7) – mchepuko unaotamanisha lakini wenye maafa – bali ni kuhusu mafundisho bayana ya ufalme ambayo yameenea katika Maandiko yote. Hoja yangu ni hii kwa urahisi: Biblia imejaa mafundisho kuhusu Ufalme wa Mungu, na Kanisa limeyakosa kwa kiasi kikubwa. Lakini katika mpango wa Mungu huenda sasa tumefikia wakati ambapo habari njema za Ufalme zinaweza kusikiwa na kueleweka kuliko wakati mwingine wowote. Hili halitokani na mtu yeyote, si kwa hekima yoyote au ufahamu wa kibinadamu, bali kwa kazi ya Mungu mwenyewe katika siku zetu, kuleta ufahamu mpya wa ufalme. Hivyo mada ya kitabu hiki ni: Ufalme wa Mungu katika Maandiko na Maana yake Kwetu Leo. Ufalme wa Mungu ni uzi muhimu katika Maandiko, unaounganisha Biblia nzima pamoja. Sio mada pekee inayoiunganisha, wala haipaswi kuchukua nafasi ya mada zingine ambazo ni za kibiblia kabisa. Hata hivyo, bado ni mada muhimu sana, hasa katika nyakati za leo. Na namna inavyorejea kwa nguvu hivi karibuni katika Kanisa, naamini, ni mojawapo ya matukio muhimu sana ya karne hii! Mara unapoanza kuangalia katika Maandiko, mada ya utawala wa Mungu au Ufalme inajitokeza kila mahali! Chukua mfano niliokutana nao hivi majuzi katika usomaji wangu binafsi: Ee Bwana, kazi zako zote zitakushukuru, Na wacha Mungu wako watakuhimidi. 11Wataunena utukufu wa ufalme wako, Na kuuhadithia uweza wako. 12 Ili kuwajulisha watu matendo yake makuu, Na utukufu wa fahari ya ufalme wake. 13 Ufalme wako ni ufalme wa zamani zote, Na mamlaka yako ni ya vizazi vyote. ~ Zaburi 145:10-13

Made with FlippingBook - Online catalogs