The Kingdom of God, Swahili Student Workbook

1 9 6 /

UFALME WA MUNGU

Ufalme Wako Uje! Usomaji kuhusu Ufalme wa Mungu (muendelezo)

5. Y esu alikuwa mtangazaji wa kwanza wa Injili, na aliitangaza kwa maneno ya Ufalme wa Mungu (Mk. 1:14-; Mt. 4:23; 9:35; 24:14; Lk 20:1). Habari njema ni kuhusu utawala wa Mungu. Bila shaka hii ni sitiari, taswira ya maneno inayoelezea ukweli wa kina. 6. M afundisho ya Yesu kuhusu Ufalme wa Mungu kama tutakavyoona, yanaamua muundo wa msingi wa mafundisho yake yote, na kwa hakika muundo wa mafundisho ya Agano Jipya kwa ujumla wake. 7. K wa nini Yesu alichagua neno “Ufalme wa Mungu” ili kutangaza habari njema ya Mungu ulimwenguni pote? Sababu mbili za msingi: a. Ilikuwa kibiblia. Ingawa kifungu cha maneno “Ufalme wa Mungu” hakipatikani kamwe katika Agano la Kale (labda mara moja katika 1 Nyakati 28:5), wazo hili liko kila mahali katika Agano la Kale. Mungu daima na kila mahali katika Agano la Kale ni Mfalme, hasa katika manabii. Mara zote Ufalme wake haurejelewi kama uliokamilika katika ulimwengu huu wenye dhambi. Kimsingi mkazo mkubwa katika Agano la Kale, unaoelezwa katika mamia ya njia na mifano tofauti ya maneno, ni juu ya wakati ujao wa Mungu, utawala unaokuja. Tumaini la Agano la Kale ni kwamba Mungu mwenyewe atakuja na kuleta wokovu kwa watu wake na hukumu/maangamizi kwa adui zake. (Ona k.m. 1 Nyakati 29:11; Zab. 22:28; 96:10-13; 103:19; 145:11 13; Isa. 25-; 65- ; Dan. 2:44; 4:3, 34; 6:26; 7:13-, 27). b. Ilieleweka na kuwa na maana kwa Wayahudi wa Palestina ya karne ya kwanza ambao aliwatangazia Habari Njema. Kwa hakika, maneno “Ufalme wa Mungu” yalikuwa yamekuzwa sana katika miaka 400 kati ya Agano la Kale na ujio wa Yesu. Ufalme wa Mungu sasa uliweka katika muhtasari tumaini zima la Agano la Kale! Wayahudi wa karne ya kwanza walikuwa wakimtazamia Mungu kuja kama mfalme na kutawala ulimwengu mzima, akiwaangamiza adui zake na kuwapa baraka zake zote watu wake, Israeli. Dhana hii ilikuwa na maana hasa kwa Wayahudi ambao, kwa upande mmoja, waliamini kwa nguvu kwamba Mungu wao Yahweh ndiye Mungu wa pekee wa kweli aliyetawala ulimwengu wote; na ambao, kwa upande mwingine, walikuwa wamepitia zaidi ya miaka 700 ya utawala wa kigeni katika mikono ya watawala wa kipagani kuanzia na Ashuru, kisha Babiloni, kisha Uajemi, kisha Uyunani na hatimaye Rumi. Yesu kamwe hawafafanulii maana ya Ufalme wa Mungu, kwa sababu

Made with FlippingBook - Online catalogs